Goli la Mkono v Peoples Power

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye

GOLI la mkono. Kwa mpira wa miguu, goli linalotambuliwa huwa ni lolote lile, kwa maana ya lililofungwa kwa njia yoyote ile isipokuwa tu, kwa mkono.

Kwa hivyo, katika mchezo huu, ule mpira unapoingizwa kwenye nyavu kwa kutumia mkono, hakika haihesabiki kuwa ni goli halali. Hilo huitwa goli haramu. Mwamuzi mwenye akili analipuuza kwa kupiga filimbi ya mpira kuanza golini badala ya kwenye mstari wa katikati ya kiwanja.

Kwa goli kama hili, katu mwamuzi hathubutu kuanzisha mpira mstari wa katikati ya kiwanja. Akithubutu huwa mchuro na huandaliwa adhabu.

Sawasawa? Goli la mkono.

Ni kweli huyu Nape anamaanisha goli wanalotaka chama chao kilipate na kutangazwa kimeshinda kura?

Duh, kumbe mchezo ushachezwa.

Au tuseme mwamuzi ameshaumuwa sikio. Waumaji sikio mwamuzi, ni wapangaji, wagharamiaji na haohao washindani. Lahaula wallaakuwatta!

Nimekuwa nikisema imezoeleka Zanzibar. Mechi inachezwa upande mmoja ukiamini lazima ushinde, hata kwa goli haramu. Komandoo Dakta Salmin alikiri ushindi huu – 50.2 Vs 49.8.

Akaita maripota pale Maisara – baada ya mzee mwenziwe Ali Ameir Mohamed kurufahia goli la mkono akiwa alishatishia kutoyatambua matokeo – na kuufurahia ushindi haramu na kuapa kuunda serikali peke yake akijiaminisha, “the winner takes it all.”

Dakta alitamba hana sababu ya kuunda serikali ya ushirikiano na Chama cha Wananchi (CUF). Inasemwa alishauriwa na Mwalimu Nyerere, baada ya kuarifiwa na wanaume kuwa Kafu juu.

Ilikuwa uchaguzi mkuu 1995 – wa kwanza baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchi, tena safari hii siasa, kinyume na ilivyokuwa miaka yote, ikifanywa kisheria ni jambo la Muungano.

Ujue hii khabari ya goli la mkono si mpya nchini.

Tangu wakati ule, kwa Zanzibar, goli la mkono. Ndio maana yake. Ndo ukamsikia Maalim Seif akisema hajawahi kushindwa uchaguzi Zanzibar?

Mbona hashitakiwi? Wanaume kimya. Mimi najua, jiulize kwanini hawamshitaki. Si somo la leo.

Watanzania mpo? Watu hawa kwa ulevi wa madaraka, wanaota ushindi wa nguvu. Yaleyale “… hatutoi kwa vijikaratasi labda nao wapindue.” Eti nini… kupindua?

Ndio, wakifunga kwa mkono wapinduliwe. Lakini kweli, majeshi wanaoabudu Sisiem (shukurani Kicheere) watapindua? Wasijaribu, mapinduzi mapinduzi tu, yanayokubalika ya Mola muumba tu, anajua ndio ufumbuzi.

Ila kule Mexico fainali za 1986 Mungu alisingiziwa eti goli la Maradona dhidi ya Brazil lilikuwa la mkono wa Mungu.

Husema mie, asiyeijua Sisiem asiombe.

Kiongozi atasemaje vile? Kisheria goli la mkono haramu, wao wanasema hata hilo washinde tu.

Mimi nimecheza mpira huu, hata juzi rafiki yangu alinitumia picha tulipocheza uwanja wa Chuo cha Ualimu Mtwara na Klabu ya Waandishi Mtwara.

Nilitoka hoi. Lakini tulicheza, ila wale vijana walitufunga goli mojawapo la mkono. Tungefanyeje; uwanja wa kwao, refa wao, tena wapo kwao, muda waliamua wao. Tusingekubali unafikiri tungeondoka Mtwara?

Niliwaambia wahariri wenzangu sitaki kula samaki-nchanga ugenini. Tuwaache wafurahie ushindi haramu. Siku hazigandi watakuja Dar.

Bahati nzuri kina Yusufu Kulangwa, Jesaya Kwayu, barubaru Kulwa Karedia na jasiri Eric Mkuti, walikubali maana hata kaka Maugo naye alishasema hakujiandaa kula samaki-nchanga.

Magoli haramu hayakubaliki hata Afrika. Lakini upinzani wakishafungwa, imetoka. Hawakubaliki kwa majeshi kama wakitaka mapinduzi.

Natahadharisha safari hii Zanzibar wanaimba mwaka wa uamuzi – wakinyang’anywa wakatae. Tanganyika vilevile, UKAWA wanajipanga kuzuia magoli haramu.

Sisiem wakishasema, wanamaanisha. Lakini Tanzania inaweza kukopa Nigeria. Kupishana kwa amani.

Kuota goli la mkono ina maana mipango mibivu. 1995 si 2015, Watanzania wameamka na kuamini “Mabadiliko sasa.”

Ends.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s