Ukawa: NEC inatuvurugia mipango majimboni

“Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” Mbowe
“Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” Mbowe

Dar es salaam. Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameishukia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushindwa kutangaza mgawanyo wa majimbo, akisema kuchelewa huko kunavuruga mipango yao.

Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, imekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais hadi diwani na viongozi wa vyama hivyo wameshakutana mara kadhaa kuzungumzia kugawana majimbo kulingana na nguvu ya chama kwenye eneo husika.

Hata hivyo, vimeshindwa kumalizia kazi hiyo kutokana na kutokamilika kwa mgawanyo wa majimbo kama NEC ilivyoahidi Mei 12 kuwa majimbo mapya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 yangetangazwa Juni 30.

Akizungumza jana, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema aliitupia lawama NEC akisema wakati huu ilitakiwa kuwa imeshamaliza suala la majimbo na kushughulikia mambo mengine.

“Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” alisema Mbowe.

Akizungumzia ukimya wa kutangaza majimbo hayo licha ya kusema ingefanya hivyo Juni mwishoni, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema hadi sasa Tume hiyo haijakamilisha ugawaji wa majimbo lakini bado wanaendelea na mchakato huo.

Alisema Tume yake imeamua kugawa majimbo hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikanaji  wa mawasiliano, hali ya kijiografia na kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2010.

Jaji Lubuva pia alisema Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo moja na jingine, mawasiliano ya simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika.

Wakati ikisuasua kutangaza majimbo mapya ya uchaguzi, NEC pia inakabiliwa na kibarua kingine cha kumalizia uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Kazi hiyo imekumbwa na matatizo kadhaa na inatakiwa ikamilishwe katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa mashine zinazotumika za teknolojia ya mfumo wa kuchukua alama na taswira za mpigakura (Biometric Voters Registration).

Jaji Lubuva alisema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo ni makubwa, jambo ambalo alisema linatokana na ongezeko la watu nchini.

Ugawaji wa majimbo unatakiwa kufanyika mara kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s