Shein: Watakaoivuruga Zanzibar watakiona

Raisi wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akikabidhi fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CCM kwa katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Vuai Ali Vuai, baada ya kukamilisha taratibu za kutafuta wadhamini katika Mikoa ya Zanzibar
Raisi wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akikabidhi fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CCM kwa katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Vuai Ali Vuai, baada ya kukamilisha taratibu za kutafuta wadhamini katika Mikoa ya Zanzibar

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wanasiasa Visiwani kuacha kutumia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kama ngao ya kuvuruga amani kinyume na madhumuni ya kuanzishwa kwake mwaka 2010.

Amewataka wanasiasa Zanzibar kuacha tabia ya kutumia SUK kama ajenda ya kisiasa bila ya kuzingatia kuwa kitendo hicho kinaweza kuifikisha nchi katika mazingira magumu na kuhatarisha amani na mshikamano kwa wananchi wake.

Akizungumza na wanaCCM muda mfupi baada ya kurejesha fomu ya kuwania tena urais wa Zanzibar kwenye Viwanja vya CCM Kisiwandui, Dk Shein alisema hilo halitaangalia sura.

Aliwataka vijana kutojiingiza katika mambo yasiyowahusu kwa kuepuka kutumiwa na makundi ya wanasiasa wenye malengo na mitizamo ya kuvuruga amani na mshikamano kwa wananchi wake.

Alisema mtu yeyote atakayefanya vurugu bila ya kujali cheo na dhamana yake, ataadhibitiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa mujibu wa sheria za nchi kwa lengo la kuhakikisha nchi inamaliza shughuli za Uchaguzi Mkuu ikiwa katika mazingira ya amani na kutaka siasa za kistaarabu kuchukua nafasi yake.

Akiwa amesindikizwa na viongozi waandamizi wa Serikali, Dk Shein alisema: “Lazima tukumbuke kuwa Zanzibar siyo mali ya mtu binafsi, bali ni nchi ya watu wote. Hatuwezi kuendelea kuvumilia watu wanaokesha wakipanga kuhujumu amani ya nchi yetu kwa kisingizio kuwa wapo katika SUK.

“Ni lazima wote tutii Katiba na sheria… hata mimi Rais sipo juu ya sheria seuze watu wengine?” Alisema iwapo CCM itampitisha kuwania nafasi hiyo na wananchi wa Zanzibar kumpatia ridhaa ya kuwaongoza, ataendelea kuisimamia Serikali kwa uadilifu mkubwa ikiwamo kuendeleza misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Hiki ni kivumbi. Kati ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania urais kupitia CCM, anatakiwa kubaki mmoja tu na mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu unafungwa kesho. Kuimarisha uchumi kwa kutumia mbinu mbalimbali, kupambana na rushwa na ufisadi, kuboresha elimu, kukuza ajira kwa vijana na kuboresha uwajibikaji ni baadhi ya ahadi zilizotawala na makada 42 waliochukua fomu.

Hadi sasa ni kada mmoja tu, Hellen Elinawinga ametangaza kutoendelea na mchakato huo.

Gazeti la Mwananchi linapitia ahadi hizo kwa kifupi.

Samweli Sitta

Waziri huyo wa Uchukuzi ameahidi kupambana na rushwa, kutenganisha uongozi na biashara na kila mara amekuwa akisisitiza kuwa: “Nitahakikisha inaandaliwa sheria maalumu ambayo itawalazimisha watu kuchagua kati ya biashara na uongozi.”

Dk Titus Kamani

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ameahidi kupambana na changamoto za afya, ajira na uchumi. Jingine ni kuangalia makundi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, wanawake na wastaafu.

Profesa Sospeter Muhongo

Mbunge wa Kuteuliwa na Rais ameahidi kukuza uchumi kwa kusimamia mafuta, gesi, umeme na elimu ili kuwakwamua wananchi katika lindi la umaskini. Pia kukuza uchumi wa nchi kwa asilimia 7.5 hadi asilimia 10 mpaka 15 kwa kipindi cha miaka mitano au 10.

Edward Lowassa

Mbunge wa Monduli amepania kuinua vijana katika ajira, kusimamia Muungano, kuinua elimu na uchumi wa nchi kupita rasilimali za ndani. Pia, kutatua migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji. Katika michezo ameahidi, kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika ramani ya dunia na kwamba ataweka mkazo zaidi katika mchezo wa riadha.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s