Wasomi, wananchi wamshukia Kinana

Katibu Muu wa CCM Abdulrahmani Kinana,akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza juzi.
Katibu Muu wa CCM Abdulrahmani Kinana,akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza juzi.

Dar es Salaam. Kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwa wabunge wa chama hicho wanaunga mkono kila hoja inayowasilishwa na Serikali bila kutathmini matokeo yake, imekosolewa na wasomi na wananchi waliosema amechelewa, huku wabunge wake wakikiri udhaifu.

Kinana, ambaye tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo amekuwa akikosoa utendaji wa mawaziri na maofisa wengine wa Serikali, juzi alipokuwa akihitimisha ziara zake mjini Mwanza, alikosoa hata mfumo wa CCM wa kumfanya Waziri Mkuu kuwa kiongozi wa wabunge.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wachambuzi hao walisema kuwa kauli hiyo imechelewa kwa kuwa hakuna dalili za chama hicho kubadilika kutokana na mifumo, utamaduni na utawala waliopitia viongozi wengi wa CCM.

Profesa Mpangala: CCM iondolewe

Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), alisema CCM inatakiwa ifanye vitu viwili ili kuwe na mabadiliko anayoyataka Kinana.

“Cha kwanza itoke madarakani ili ikajipange upya, na cha pili kama itabaki madarakani ihakikishe inamchagua kiongozi shupavu asiyeyumbishwa na mifumo iliyopo ya chama,” alisema Profesa Mpangala.

Alisema viongozi wa sasa wa CCM wamekuwa wakituhumiwa kwa rushwa, ufisadi tofauti na siku za nyuma alizosema hata kama rushwa ilikuwapo ilikuwa kwa kiwango kidogo.

“Chama kimebadilika sana, kimekuwa na viongozi wabinafsi, wanaotaka maendeleo yao binafsi badala ya wananchi waliowachagua,” alisema.

“Kauli ya Kinana inaonyesha wazi anataka mabadiliko na ni wazi kuwa chama hicho kinahitaji mabadiliko ambayo hayawezi kufikiwa bila kufuata hizo njia mbili. Watoke ili watambue walikuwa wanakosea wapi kwa kujifunza kwa wenzao watakaoshika dola au kwa dola nyingine, au wabaki kwa kumuweka kiongozi shupavu asiyeyumba.

“Ninachokiona na kukisema wazi ni kwamba Kinana hawezi kukibadilisha chama kwa hatua kilichofikia… rushwa, ufisadi, umimi vimekuwa ndiyo dira. Viongozi wamepoteza mwelekeo, wamejisahau, wanahitaji muda wa kurekebisha walipokosea.”

Mbunda: Wabunge CCM si makini

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda aliungana na Kinana kukubaliana kuwa wabunge wa CCM si makini na ndio maana wanapitisha sheria ambazo ni kandamizi kwa wananchi.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s