NEC yaahirisha uandikishaji wapigakura Dar

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba.
                                     Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba.

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha kwa muda uandikishaji wa wapigakura katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa. Uandikishaji huo unaofanywa kwa teknolojia inayochukua alama na taswira za mpigakura ‘Biometric Voters Registration’ (BVR)) ulipangwa kuanza Julai 4 hadi 16 kwa Dar es Salaam na Juni 25 kwa Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kuwa kazi hiyo imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vinavyotumika kuandikisha wapigakura.

Alisema vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa kutumika Dar es Salaam bado vinatumiwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

“Mwitikio umekuwa mkubwa ndiyo maana tumeamua kusogeza mbele tarehe ili wamalizie huku tukiendelea kusubiri vifaa. Tunataka vikija tuishambulie Dar es Salaam kwa kipindi kifupi,” alisema Mallaba.

Mallaba alisema tarehe ya kuanza tena kwa kazi hiyo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani itatangazwa na NEC baada ya kupata vifaa kutoka mikoa itakayokuwa imekamilisha uandikishaji.

“Ninaomba wananchi wafahamu kuwa mwezi uliokuwa umepangwa na NEC kukamilisha zoezi hilo utabaki kuwa Julai. Tarehe tu ndiyo itabadilika,” alisema na kusisitiza kuwa wanataka uandikishwaji kwa jiji hilo uwe wa kipekee ukiwa na vifaa vya kutosha kutokana na idadi kubwa ya watu. Aliwataka wananchi wote wa mikoa hiyo miwili kuwa watulivu wakati huu.

Mnyika akerwa

Akizungumzia hatua hiyo, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema NEC imedhihirisha hoja aliyowahi kuitoa bungeni kwamba Bunge liahirishwe ili wajadili suala hilo kwa dharura.

“Kuna udhaifu mkubwa kwa upande wa NEC na Serikali kuhusu BVR… hata baada ya madai kwamba umerekebishwa lakini ukweli ni kwamba hali ni tete hata katika maeneo mengine ambayo uandikishaji unaendelea,” alisema Mnyika.

Alieleza kuwa Dar es Salaam ndiyo itakayoamua mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kutoka na idadi kubwa ya wapigakura.

Alidai kwamba kubadilishwa huko kwa ratiba kutatoa mwanya kwa CCM ambayo ilishasema kupitia kwa Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi) kuwa inajiandaa kufunga goli la mkono kufanya hujuma.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s