Zanzibar shirikianeni mvuke uchaguzi salama

Ni siku ambayo wawili hawa wailipeana mikono baada ya kazi refu na kubwa iliyofanywa na kamati ya watu sita ya kuleta maridhiano ya Zanzibar baada ya siasa za uhasama na chuki za miaka kadhaa
Ni siku ambayo wawili hawa wailipeana mikono baada ya kazi refu na kubwa iliyofanywa na kamati ya watu sita ya kuleta maridhiano ya Zanzibar baada ya siasa za uhasama na chuki za miaka kadhaa

Gazeti hili jana lilikuwa na habari iliyosema mawaziri wa serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) na wawakilishi kutoka CUF, walitoka kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho vya ukazi wa Zanzibar na uandikishaji wapigakura.

Madai hayo yalifafanuliwa vizuri na mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu kwamba uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapigakura umekumbwa na vurugu zilizotokana na kutumika kwa vyombo vya dola vinavyolazimisha watu wasio na sifa kuandikishwa.

ko5

Mei 14, gazeti la Mwananchi Jumapili liliandika habari kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kwamba alikwenda Dodoma kuonana na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kulalamikia vitendo hivyo kwa kuwataka waingile kati.

Yote hayo kwa ujumla wake tunayaita ni viashiria vibaya vya kisiasa hasa tukiangalia ilikotoka Zanzibar, ambayo kwa muda mrefu imekuwa na historia ya siasa za chuki na uhasama wa kulipiza kisasi, hali iliyowafikisha wananchi wake hadi kutouziana bidhaa madukani na kutozikana.

hqdefault

Sote ni mashuhuda kuwa Zanzibar imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa hasa wakati wa utawala wa Dk Salmin Amour , aliyeongoza kuanzia 1990 mpaka Oktoba 2000. Kipindi hicho CUF iliwahi kutangaza kutomtambua Rais Salmin, wakidai wameporwa ushindi.

Tungependa kutahadharisha yale yaliyojitokeza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, kwa baadhi ya Wazanzibari kuikimbia nchi na kwenda kuwa wakimbizi eneo la Shimoni, Mombasa nchini Kenya, yawe fundisho kwa kutuongoza kwenye siasa za maelewano.

timu-kuu1

Vyama viwili vya CCM na CUF vimekuwa vikiumiza vichwa vya Watanzania na wasio Watanzania, kutokana na migogoro ya kisiasa isiyoisha hasa wakati wa uchaguzi, na hali inayoanza kujionyesha sasa ni dalili za kuchimba kaburi la historia ya siasa za chuki na uhasama wa kulipiza kisasi, vilivyozikwa kutokana na mazungumzo ya faragha ya Novemba 5, 2009, kati ya katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Amani Abeid Karume, alipokuwa Rais wa Zanzibar.

Kabla ya maridhiano ya Seif na Karume yaliyozaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), huko nyuma kumekuwepo juhudi nyingi za kurekebisha hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo ya kwanza ya kutafuta suluhu ya mpasuko wa kisiasa kati ya vyama vya CUF na CCM yalianza mwaka 1999, ambayo yalisimamiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Chifu Emeka Anyaoku.

Wote ni mashahidi kwamba mwafaka huo haukufua dafu, lakini Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani aliviingiza tena vyama hivyo vya CUF na CCM katika mazungumzo ya mwafaka baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, kutokana na CUF kutangaza kutomtambua Rais Karume kwa kile walichodai kuporwa ushindi, hata hivyo mazungumzo yote hayakufanikiwa kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

Tunaamini kwamba maridhiano kati ya Maalim Seif Sharif Hamad na Amani Abeid Karume, yameweza kuviweka visiwa hivyo katika hali ya amani, utulivu na maelewano. Wazanzibari walisahau vyama vyao na kujali uzanzibari wao, lakini vuguvugu la sasa linalotaka kuibuka tunaona ni kama vile kuirejesha Zanzibar katika siasa za uadui.

Ni imani yetu kwamba ndugu zetu wa Zanzibar wataendeleza maridhiano yaliyowafikisha katika kuunda SUK, na kwamba mchakato wa uchaguzi na hadi uchaguzi wenyewe hautakuwa chanzo cha kuwarejesha kwenye siasa za uhasama na chuki zilizopitiliza. Tunasema Zanzibar shirikianeni mvuke salama kwenye uchaguzi. Kila upande ufanye majukumu yake inavyotakiwa.

 Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s