Hapatoshi CCM Dodoma

Fundi akisugua ukuta kabla ya kuanza kupaka rangi makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya vikao vya kamati ya maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho vitakavyo kaa mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuteua majina ya wagombea kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho.
Fundi akisugua ukuta kabla ya kuanza kupaka rangi makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya vikao vya kamati ya maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho vitakavyo kaa mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuteua majina ya wagombea kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho.

Dodoma. Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma. Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Hekaheka za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya maadili, Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, zimeanza kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni na hoteli zikiwa zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma, umebaini kuwa nyumba za kulala wageni na hoteli zimejaa kuanzia Julai 8 hadi 12, mwaka huu.

Hali hiyo imewafanya watu wanaotaka kupanga katika nyumba hizo kuulizwa wataondoka lini, ili tarehe za ‘booking’ zisigongane.

“Utaondoka lini, maana CCM wamechukua nyumba zote hapa kati ya Julai 8 hadi 12,” alisema mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni ya Kiramiya.

Chanzo cha habari kutoka katika ofisi ya CCM, kimesema wajumbe wote 2,448 wa mkutano mkuu wamepata maeneo ya kulala kwa siku watakazokuwa mjini hapa.

Hata hivyo, chanzo hicho kimedokeza kuwa changamoto imekuwa katika kupata malazi ya wageni 600 waalikwa, watakaokuja kuhudhuria mkutano mkuu huo utakaofanyika katika ukumbi mpya wa chama hicho.

“Katika maeneo mengi tuliyokwenda tulikuta hoteli zimechukuliwa na wapambe wa wagombea wa urais ambao tayari wamelipia siku watakazokaa mjini hapa,” alisema mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya CCM na kuongeza:

“Hivi sasa wenzangu wako mtaani wanatafuta nyumba nyingine.”

Alisema hali imekuwa ngumu kutokana na wapambe wa wagombea ambao hadi sasa wamefikia 39 kuchukua vyumba vingi na kuvilipia kabisa, tofauti na CCM iliyopanga kuanza kulipia malazi hayo leo.

Ukarabati

Katika hatua nyingine, mafundi wameonekana wakifanya marekebisho katika majengo ya makao makuu ya chama hicho hasa jengo maarufu la ‘White House’ ulipo ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Chanzo: Mwananchi

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s