Mawaziri Zanzibar wasusia bajeti

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Ahmed Nassor Mazrui, akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habarai katika Ofisi za CUF Vuga baada ya Mawaziri wote wa CUF na wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia Chama hicho kususia kupitisha bajeti Kuu ya serikali. Kutoka ni   Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakary Khamis, Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Abdillah Jihadi, Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji, Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo said ali Mbarouk na Waziri wa Nchi Ofisi ya makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Fereji.
Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Ahmed Nassor Mazrui, akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habarai katika Ofisi za CUF Vuga baada ya Mawaziri wote wa CUF na wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia Chama hicho kususia kupitisha bajeti Kuu ya serikali. Kutoka ni Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakary Khamis, Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Abdillah Jihadi, Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji, Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo said ali Mbarouk na Waziri wa Nchi Ofisi ya makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Fereji.

Zanzibar. Mawaziri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na Wawakilishi kutoka CUF jana walitoka kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho vya ukazi wa Zanzibar na uandikishaji wapigakura.

Muda mfupi baada ya tukio hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitoa taarifa yake ikisema kitendo cha mawaziri wa CUF kutoka kwenye kikao cha bajeti ni kuvunja katiba, kwa kuwa wameshindwa kuheshimu kiapo cha utii katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Mawaziri hao walitoka nje ya kikao hicho muda mfupi baada ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji kusimama na kutoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji wa SUK katika kusajili na kutoa vitambulisho hivyo vinavyotumika katika kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Wapigakura.

Wakati wawakilishi hao wanaondoka ndani ya ukumbi, wenzao wa CCM walikuwa wakipiga makofi huku wakiimba “CCM, CCM, CCM”, na baadaye baraza kuendelea na muswada wa kupitisha mapato na matumizi ya bajeti ya mwaka 2015/2016.

Mawaziri waliohudhuria mkutano huo ni Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Waziri wa Sheria na Katiba, Fatma Abdulhabib (Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais), Abdilahi Jihadi Hassan (Mifugo na Uvuvi) na Haji Mwadini Makame (Ardhi, Makazi, Maji na Nishati).

“Tumeamua kutoka ndani baada ya kuona wenzetu tuliowaamini, wametubadilikia. Hawana nia njema ya kuendesha serikali ya pamoja,” alisema makamu mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji alipoongea na waandishi baada ya kutoka kwenye ukumbi huo.

“Wameanzisha Serikali ndani ya Serikali na sasa wanawanyima haki wananchi kinyume na katiba.”

Duni alisema kwa miaka mingi wananchi wamekuwa wakizungushwa kusajiliwa na kupewa vitambulisho vya ukazi, hali inayowaweka katika hatari ya kupoteza haki zao za kijamii, ikiwa ni pamoja na fursa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo, alisema uamuzi wao haujavunja katiba ya Zanzibar na kwa hiyo wataendelea na shughuli za Serikali kama kawaida.

Alidai kuwa kazi ya uandikishaji wapigakura kwenye Wilaya ya Magharibi, Unguja imetawaliwa na vitisho na kwamba watu wasiojulikana wamekuwa wakionekana wakiwa na silaha za moto na kujifunika vitambaa usoni mithili ya maninja na wengine kuvaa vinyago.

“Katika maisha yangu sijawahi kuona askari anayekwenda kulinda akificha uso na huu ni mkasa mpya duniani. Huwezi kumlinda raia kwa silaha za moto wakati yeye hana chochote zaidi ya mikono yake,” alisema Duni.

Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuna vijana wamekwama kuandikishwa na kuitaka Serikali kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vitambulisho vya ukazi.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

One Reply to “Mawaziri Zanzibar wasusia bajeti”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s