Dk Shein:Nitawashinda wapinzani Zanzibar

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba udhamini wa wanachama wa CCM kwa ajili ya kuteuliwa kuwania ugombea urais wa Kisiwa hicho baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Zanzibar jana. Picha Talib Ussi
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba udhamini wa wanachama wa CCM kwa ajili ya kuteuliwa kuwania ugombea urais wa Kisiwa hicho baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Zanzibar jana. 

Zanzibar. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Ali Mohamed Shein jana alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kuteua tena kugombea urais wa Zanzibar huku akitamba kuwa ataendeleza wimbi la ushindi dhidi ya wapinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Alisema iwapo chama chake kitampitisha na kupewa ridhaa na wananchi, atahakikisha Serikali yake inafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na uwazi.

Akisindikizwa na makada wa CCM, Dk Shein alisema katika kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano inayomalizika, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imefanikiwa katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk Shein aliwaambia viongozi wa mikoa sita ya kichama kuwa wakati anaingia madarakani mwaka 2010, aliweka misingi imara ya utawala bora kwa kufanya tathmini ya utendaji kwa kukutana na kila wizara baada ya miezi mitatu kuangalia matatizo na mafanikio.

“Kama kawaida yangu napenda kuwahakikishia kuwa nitaongoza Serikali yenye uwazi, uwajibikaji na yenye uwezo wa kutimiza majukumu yake na kulinda misingi ya haki za binadamu, sheria na Katiba,” alisema Dk Shein.

Alisema lengo kubwa la serikali yake ni kujenga uchumi imara na kuendeleza malengo ya kuimarisha sekta ya kilimo, uvuvi, viwanda na sekta ya uwekezaji ili kuinua Pato la Taifa na wananchi wa Zanzibar.

Alisema ni jambo la faraja kuona uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia saba kutoka asilimia 2.6 ya mwaka 2010, huku uwezo wa ukusanyaji mapato ukifikia Sh35 bilioni kutoka Sh13.5 bilioni kwa mwezi mwaka 2010.

Alisema iwapo CCM itampatia tena ridhaa na kuchaguliwa na wananchi kuendelea na wadhifa huo wa urais, atahakikisha anaendelea kulinda misingi ya Mapinduzi na Muungano.

“Kuna watu wachache wanautia chokochoko Muungano na Mapinduzi yetu, msiogope, tutawashughulikia kwa mujibu Katiba na sheria bila ya kutumia nguvu,” alisema na kuibua shangwe za CCM…CCM…

Alisema ili Zanzibar iweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo baada ya uchaguzi mkuu, atahakikisha amani na utulivu vinapewa nafasi kubwa.

Alisema hatakuwa na mzaha katika kusimamia misingi ya utawala wa sheria na hakuna mtu ambaye ataonewa katika uongozi wake… “Mimi ni muumini wa Kiislamu, sitomdhulumu mtu, najua kwamba kumdhulumu mtu ni dhambi, nitatenda haki na yeyote atakayeleta chokochoko na Zanzibar sitamuachia kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.”

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s