Chema chajiuza, kibaya chajitembeza- Jaji Ramadhan

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani akiondoka makao makuu ya CCM Dodoma jana, baada ya kuchukua fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho
Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani akiondoka makao makuu ya CCM Dodoma jana, baada ya kuchukua fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho.

Dodoma. Jaji Mkuu wa zamani wa Tanzania, Augustino Ramadhan, mmoja wa watu waliokuwa wakitajwa kuwa na nia ya kuingia kwenye mbio za urais, jana alichukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo, akisema “chema chajiuza, kibaya chajitembeza”.

Jaji Ramadhan ni mmoja wa makada wengi wa CCM ambao wamekuwa wakitajwa kwa muda mrefu kuwa wanaweza kuomba ridhaa ya CCM kuwania nafasi hiyo ya kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kuachia ngazi mwishoni mwa mwaka.

Ubashiri huo ulitimia jana wakati brigedia huyo wa zamani alipofika ofisi za makao makuu ya CCM mjini hapa, akisindikizwa na familia yake, kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya wanachama kuwania urais zikiwa zimesalia siku 15.

Jaji Ramadhan, ambaye ni rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, alifika katika ofisi hizo saa 6:30 mchana akiwa ameambatana na mke, watoto wake watatu, mdogo wake na msaidizi wake.

“Hao ndio watu niliokuja nao sikutaka makeke kwa sababu waswahili wanasema chema chajiuza, kibaya kinajitembeza,” alisema baada ya kuwatambulisha watu alioongozana nao.

Jaji Ramadhan, ambaye hakutaka kuzungumzia mikakati yake lakini akakaribisha maswali ya waandishi wa habari, anakuwa kada wa 36 kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo, ambayo kama atapewa atakuwa pia mwenyekiti wa CCM.

Akijibu maswali , Jaji Ramadhan alisema: “Nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wenzangu, tuende huko tunakotaka, tujenge Taifa tunalolitaka na kunyanyua hali za binadamu. Nimefanya hivyo katika masuala ya haki nimekuwa Jaji na Jaji Mkuu Zanzibar na Muungano,” alisema Jaji Ramadhan ambaye anajulikana zaidi kutokana na hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila ya kutaka mahakama itambue mgombea binafsi.

“Hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuniambia kwamba nilichukua rushwa au huyu nilimuangamiza au nilimwonea mtu sasa. Nilipata nafasi hiyo na leo nataka nafasi kubwa zaidi ya kiuongozi nchi nzima.”

Katika kesi hiyo, Jaji Ramadhan na jopo lake walisema uamuzi huo unatakiwa ufanywe na Bunge, na kuibua mjadala mkubwa.

Jaji Ramadhan alikuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Tanu, Agosti 1969 wakati akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alipomaliza alijiunga na Jeshi la Wananchi (JWTZ), huku akiwa mwanachama wa Tanu.

Aliendelea kuwa mwanachama wa Tanu hadi mwaka 1992 wakati mabadiliko ya Katiba yalipozuia wanajeshi na majaji kuwa wanachama wa vyama vya siasa baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, lakini alirejea CCM baada ya kustaafu mwaka 2011.

“Upande wa Jeshi nilikaa hadi nilipokuwa brigedia na nilitoka tena kwa sababu ya sheria. Katiba ilipoleta hoja ya mtu kutokuwa mwanajeshi na Jaji nikaamua kuacha,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s