Ali Karume, Mwanadiplomasia anayetegemea kubebwa na historia

Katika makuzi yake, Ali Abeid Karume hakujua kama atakuja kujulikana kama mtoto wa rais. Akiwa na miaka 14 baba yake alikuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, baada ya kuipindua Serikali iliyokuwa madarakani kwa mwezi mmoja tu, kuanzia Desemba 10, 1963 hadi Januari 11, 1964.
Katika makuzi yake, Ali Abeid Karume hakujua kama atakuja kujulikana kama mtoto wa rais. Akiwa na miaka 14 baba yake alikuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, baada ya kuipindua Serikali iliyokuwa madarakani kwa mwezi mmoja tu, kuanzia Desemba 10, 1963 hadi Januari 11, 1964.
Salma Said
Alizaliwa katika mazingira ya kawaida ya Wazanzibari katika miaka ya 50 kwenye familia ya baharia Abeid Amani Karume aliyekuwa mume wa Fatma Ali Daud (Fatma Karume). Fatma ni mzaliwa wa Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja, yeye mwenyewe anasema aliolewa na Abeid Karume akiwa binti mdogo kabisa. Huyu ndiye mama wa Ali na Amani Karume.

Katika makuzi yake, Ali Abeid Karume hakujua kama atakuja kujulikana kama mtoto wa rais. Akiwa na miaka 14 baba yake alikuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, baada ya kuipindua Serikali iliyokuwa madarakani kwa mwezi mmoja tu, kuanzia Desemba 10, 1963 hadi Januari 11, 1964.

Ali ni mtoto wa kwanza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Baada ya kuhitimu shule ya msingi, alisoma katika Shule ya Sekondari ya Tumekuja mjini Unguja. Alipomaliza shule alikwenda kufanya kazi katika Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar (ZSTC) hadi 1970 alipopandishwa cheo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo kazi aliyoifanya kwa miaka miwili.

Mama Fatma Karume akisalimiaana na Dk Shein
Mama Fatma Karume akisalimiaana na Dk Shein

Ali Karume amekuwa mwanachama wa Afro Shirazi Party tangu mwaka 1970 na hivyo mwaka 1977 Tanu na ASP zilipoungana na kuunda CCM, Ali akawa mwanachama wa CCM. Akiwa na miaka 28 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Biashara na Viwanda katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kazi aliyoishikilia kwa miaka sita (1972 – 1978) alipoomba likizo na kwenda kujiendeleza zaidi kimasomo nchini Marekani.

Ali Karume ameanza kufanya kazi za kibalozi mwaka 1989 alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Mwaka 1993 akawa Mkurugenzi wa Idara ya masuala ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania hadi mwaka 1996 alipopelekwa Ubelgiji kuwa Balozi wa Tanzania kwa nchi za Ubelgiji, Uholanzi, Luxembourg na Umoja wa Ulaya.

Amani Karume na Ali Karume
Amani Karume na Ali Karume

Mwaka 2002 Ali akawa balozi wa Tanzania katika nchi za Ujerumani, Uswizi, na Poland sambamba na kuangalia mahusiano na nchi za Austria, Jamhuri ya Chek, Slovakia, Hungary, Romania na Bulgaria.

Kuanzia mwaka 2006 Ali karume aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi za Italia, Ugiriki, Uturuki na Malta. Pia amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cyprus na Mkuu wa Mabalozi wa Tanzania. Uzoefu wa Ali Karume katika njanya za kimataifa ni mkubwa kwani amekuwa Balozi kwa zaidi ya miaka 20.

Ali Karume na urais

Hamu yake ya kugombea urais haikuanza leo, kwani mwaka 2000 alionyesha nia na kuingia katika kinyang’anyiro cha uteuzi ndani ya CCM kwa upande wa Rais wa Zanzibar lakini alijitoa katika hatua za awali na kumwachia nduguye Amani Abeid Karume.

8e9u0541

Mwaka 2005 na mwaka 2010 alijitosa katika kugombea uteuzi wa chama chake ili apeperushe bendera ya CCM kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini pia bahati haikuwa yake.

Wanavyomzungumzia wanaomfahamu

Enzi Talib ambaye alikuwa mwandishi wa habari Ofisi ya Rais, Zanzibar anamuelezea Ali Karume kuwa ni mtu mwenye kiburi na kwamba alikuwa mtundu kupita kiasi wakati wa udogo wake.

“Alikuwa mkorofi sana na ndio maana baba yake akampeleka Bara kwa Mwalimu Nyerere akatulie alikuwa na matatizo sana na kuna siku baba yake alimtandika bakora mbele za watu kwa sababu ya ukorofi wake,” anasimulia Talib.

Talib ambaye amekamata nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na sasa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais anasema sifa kubwa ambayo inatakiwa mtu awe nayo kwa mazingira ya Zanzibar ya sasa ni kuwa na uwezo wa kusimamia suala la Muungano na hadhani kama Ali anayo sifa hiyo.

Talib alishiriki katika tume zote zilizoundwa za kushughulikia kero za Muungano akiwa kama katibu anasema Mzee Karume alikuwa na uwezo na akiogopwa lakini pia alikuwa na watu wenye kumuunga mkono, lakini bahati mbaya Ali hana uwezo huo wala hana watu wa maana wanaomuunga mkono, hivyo itakuwa vigumu kusema atashughulikia suala la Muungano wakati viongozi waliokuwa wakionyesha ujasiri wameshindwa.

Wapo wanaomuunga mkono

Biubwa Amour Zahor ni mwanamke mwanamapinduzi pekee aliyeshiriki mapinduzi kikamilifu. Anamzungumzia mtoto wa mwana mapinduzi mwenzake ambaye amechukua fomu kuwania urais kuwa ni mtu asiye na mawazo mgando na kwa kuwa ameishi katika mfano wa nchi zenye maendeleo makubwa, hivyo anayo visheni nzuri ya maendeleo.

Biubwa anamwona Ali Karume kuwa ni mtu anayependa sana watu na kupokea ushauri wa kila rika, lakini ni mtu ambaye amelelewa katika siasa na kukulia katika nyadhifa mbali mbali za uongozi kwa hivyo kuongoza kwake sio jambo kubwa bali ni jambo la kawaida.

“Ali sio mtu wa tamaa na ana nia ya kweli ya kuisaidia Zanzibar kiuchumi na kuleta mabadiliko kwa sababu yeye huyu ni mwana uchumi mwenye Shahada ya Uzamili ya masuala ya Uchumi,” anasema.

Ila Biubwa anasahau kuwa Ali Karume hagombei urais wa Zanzibar bali wa Tanzania, je, anao ubavu huo?

Mara zote alizojaribu kugombea nafasi hiyo ya juu, Ali Karume alienguliwa kutokana na kuwa kura anazopata hazitoshi lakini hilo kamwe jambo hilo halijawahi kumvunja moyo, bado ana ari na ghera ya kuingia Ikulu sasa akiwa kama kiongozi na wala si kama mtoto kama ilivyokuwa katika miaka ya 60 na ya mwanzo wa 70 kabla baba yake hajauawa.

“Namuona atakuwa kiongozi mzuri, amepikika tokea udogoni ameona uongozi wa baba yake Mzee Karume lakini pia ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya nchi na uzoefu wake wa huko ughaibuni alikoishi kwa muda mrefu utamsaidia kuwa na dira yenye manufaa,” anasema Bimkubwa.

Rafiki wa karibu

Rafiki wa karibu Ali Miraji Othman anamuelezea Ali Karume kama ni kiongozi asiyependa majungu, mwenye busara na mtu ambaye anapenda kukosolewa.

“Wapo watu wengine hawapendi kukosolewa wala hawapokei ushauri wa mtu yeyote, anavyoamua yeye ndiyo hivyo hivyo lakini ni tofauti na Ali, yeye anakubali ushauri na anapenda maingiliano na watu sana kwa hivyo muda mwingi akiwa nchini anakuwa pamoja na marafiki zake,” alisema.

Pamoja na maoni mchanganyiko kuhusu Ali Karume, wapo wanaosema kuwa kwa vyovyote vile iwavyo Ali Karume ni mgeni, sio watu wengi wanaomjua hulka zake hasa kwa sababu muda mwingi ameutumia nje ya nchi, wanadhani ni mzuri zaidi katika medani ya ubalozi kuliko urais.

Kadhalika wapo wanaoona kuwa Ali Karume anaweza kupenya kwenye tundu ya sindano iwapo hoja ya kuwa mara hii ni zamu ya mgombea kutoka Zanzibar itapata mashiko, ingawa hiyo haimo katika maandiko yoyote ya kisheria wala kanuni.

Aidha Ali Miraji anasema ikiwa CCM itampendekeza Ali Karume kugombea urais na akashinda, Tanzania itashuhudia mafanikio makubwa katika uchumi kwa kuwa Ali Karume ni mwanauchumi aliyebobea.

Je, historia itambeba?

Mwaka 2000, mtoto wa pili wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar na akaongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka kumi. Kuchaguliwa kwa Amani Karume pamoja na uwezo wake wa kiuongozi kulitokana pia na historia ya Hayati Mzee Abeid Amani Karume aliyekuwa kiongozi mwenye dira na misimamo thabiti.

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “Ali Karume, Mwanadiplomasia anayetegemea kubebwa na historia”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s