Shein afungua milango kwa wawekezaji Ulaya

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein

Ujerumani. Nchi za Magharibi zimetakiwa kuongeza jitihada zaidi kuhamasisha ukuaji wa viwanda barani Afrika ili zizalishe bidhaa zinazovutia masoko ya dunia badala ya kusafirisha malighali kutoka Afrika kwenda katika nchi hizo.

Wito huo ulitolewa jana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein wakati akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Wafanyabishara wa Ujerumani wanaofanya biashara Afrika uliofanyika mjini Berlin, Ujerumani.

“Ni lazima tuangalie mbali zaidi badala ya kusafirisha malighafi kutoka Afrika na kupeleka Ulaya na Marekani. Watafiti wa nchi zetu wasaidiwe kuhamasisha na kuongeza thamani ya bidhaa kwa ajili ya masoko ya Ulaya na dunia,” alisema Dk Shein.

Dk Shein alisema wafanyabiashara na wenye viwanda wa nchi za Magharibi, ikiwamo Ujerumani, hawana budi kutumia fursa ya mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi barani Afrika pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji Zanzibar kuleta vitega uchumi vyao.

“Uchumi wa Tanzania mwaka jana ulikua kwa asilimia saba na Zanzibar ukikua kwa kiwango hicho hicho. Ukuaji wa jumla wa uchumi kwa Afrika kwa mwaka 2012 ulikua kwa asilimia 5.3,” alifafanua.

Dk Shein alitumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara hao kuwekeza Zanzibar na Tanzania kwa jumla na kuwaeleza kuwa, mbali ya kuwapo mazingira mazuri ya uwekezaji, pia kuna fursa nyingi.

“Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji miongoni mwao ni sekta ya utalii, tunawakaribisha wawekezaji kutoka Ujerumani,” alisema.

Aliongeza kuwa ni jambo la kufurahisha kuona baadhi ya wawekezaji kutoka Ujerumani tayari wameshapiga hodi nchini na kuwekeza kwenye sekta ya utalii.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s