Dk Bilal mwanafizikia anayeutaka urais

Dk Mohammed Gharib Bilal
                                                      Dk Mohammed Gharib Bilal

Na Salma Said na Nuzulack Dausen

Zanzibar/Dar es Salaam. Ni saa 4:30 asubuhi, mwandishi wa Mwananchi alipofika Mtaa wa Migombani Nje kidogo na Mji wa Zanzibar, nyumbani kwa Bi Safia Abeid Naseeb na kukaribishwa kwa heshima zote. Safia ni mcheshi, mchangamfu, mwenye kupenda kuongea.

Licha ya hali ya uzee aliyonayo,  nilimkuta bibi huyo maridadi, amevalia khanga zake akiwa kitandani, akijitayarisha kupata kifungua kinywa.

Muda huo bi Safia, ambaye ni mama mzazi wa Dk Mohammed Gharib Bilal alikuwa akijiandaa kupata staftahi yake, supu ya samaki na boflo.

“Karibu mama yangu haya asubuhi kuna nini tena umekuja kunitembelea mwanangu?” Safia alimhoji mwandishi, ambaye alijitambulisha na kueleza dhamira yake:

 “Nimekuja kukuuliza kuhusu mwanao Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye amejitosa katika kinyang’anyiro cha kutaka achaguliwe kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Bi Safia akajibu: “Ahaa, ni kweli, mwanangu alikuja hapa na kunieleza kama anataka kuingia katika uchaguzi kwa mara nyingine. Nikamuuliza; mwanangu utapata au unataka kunitia tumbo joto kama mara ile ilopita?

Maana mimi niliumwa sana na ndiyo maana sipendi mwanangu ajiingize katika mazonge haya. Lakini kama kaamua, mimi niseme nini? Namuombea Mwenyezi Mungu amvushe salama.”

Anasema kuwa alijaliwa kupata watoto tisa, lakini kati yao wanne wameshafariki dunia ambapo aliwataja ni Bilal, Maulid, Daud na Salama huku walio hai wakiwa ni Fatma, Haroub, Abeid, Said na Dk Mohammed Gharib Bilal.

“Mohamed anao ndugu zake wengine kwa upande wa baba kwa kuwa baba yake alikuwa na wake watatu, hivyo yuko Dk Hakeem na Gharib.

“Mimi napenda kumuunga mkono mwanangu kwa kile anachokipenda lakini pia sipendi apatwe na fadhaa maana mara ile mwanangu alipatwa na fadhaa kwa mambo aliyofanyiwa kule Dodoma, mimi binafsi yaliniumiza sana roho yangu,” aliongea huku akionyesha na huzuni.

 Akimuelezea mwanawe Bi Safia anasema hana marafiki wengi Zanzibar kwa sababu yeye hajaishi sana Unguja kwa kuwa muda mwingi alikuwa masomoni Marekani na pia alikaa sana Dar es Salaam alikofanya kazi.

 Anasema Dk Bilal alipata nafasi ya kwenda masomoni Marekani na akaishi huko kwa muda wa miaka mitano baadae akarejea Tanzania ambapo ndio kwa mara ya kwanza bibi huyu akasafiri hadi Dar es Salaam kwenda kumuona mwanawe huyo.

 “Nilikuwa sijawahi kwenda Dar es Salaam, lakini alipokuja mwanangu kutoka masomoni ndio nikaitwa lakini yeye alifikia kwa Mwalimu Julius Nyerere na sisi tukafikia kwenye nyumba nyingine, baadaye tukenda kuonana naye,” anasimulia.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

2 Replies to “Dk Bilal mwanafizikia anayeutaka urais”

  1. Ivo kwani mtu lazima awe rais kushawishi mabadiliko katika jamii. Wengi wa wagombea hawa wanayadhifa kubwa kwenye Chama na Serikali inayoyatawala. Hapo nyuma walishindwa kwa nini. Kwa vipi moja wao akiwa rais atafanya aonekane ni tofauti.

  2. wakati wakulaumia tu huu umeshatabiriwa na mtume (S.W.A) hakuna mmoja anaweza kuleta mabadiliko, hao wabunge na wakilishi si wa CUF wala CCM hawanawanachokifanya tutabaki ivyo ivyo kujiwekea tamaa tu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s