Nani ni nani Urais: Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad

KWA UFUPI

Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.

Historia yake

Maalim Seif Sharif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar na pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF. Maalim Seif alizaliwa Oktoba 22, 1943 huko Nyali, Mtambwe katika Wilaya ya Wete iliyoko kisiwani Pemba.

Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.

Pamoja na kufaulu vizuri sana masomo ya kidato cha sita, Maalim Seif hakwenda chuo kikuu kwa sababu serikali ilimtaka afanye kazi serikalini ili kuziba nafasi za kazi zilizokuwa wazi kutokana na kuondoka kwa wingi kwa Waingereza kurudi nchini kwao. Maalim aliajiriwa kama mwalimu kwa miaka tisa, yaani 1964 – 1972 na alifundisha Sekondari Fidel Castro iliyoko Pemba na Chuo cha Ualimu cha Lumumba kilichoko Unguja.

Mwaka 1972 aliruhusiwa kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusomea shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa, Usimamizi wa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, alihitimu shahada hii mwaka 1975 akiwa mmoja wa wanafunzi waliofaulu vizuri sana kiasi kwamba chuo kilipenda abakie kufundisha, jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Maalim Seif alianza kujifunza na hata kuingia katika masuala ya uongozi mkubwa wa serikali mwaka 1975, alipoteuliwa kuwa Msaidizi Binafsi wa Rais wa Zanzibar wakati huo (Aboud Jumbe) ambapo aliifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977. Mwaka 1977 akateuliwa kuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar na akatumika katika nafasi hiyo hadi mwaka 1980.

Mwezi Februari 1984 akateuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar (Cheo sawa na cha Waziri Mkuu wa Tanzania, kimajukumu). Maalim Seif amekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Mwinyi kama Rais wa Zanzibar, na mwaka 1985 alipochaguliwa Rais Idris Abdul Wakil kuongoza Zanzibar, bado Maalim Seif aliteuliwa kuwa Waziri Kiongozi na alishikilia wadhifa huo hadi Januari 1988 alipoondolewa katika baraza la mawaziri na baadaye kufukuzwa ndani ya CCM. Kwa hivyo, Maalim Seif amekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuanzia mwaka 1977-1988.

Tokea Maalim Seif aondolewe katika utumishi wa uongozi wa juu wa Zanzibar (akiwa mwanachama wa CCM), imemchukua miaka zaidi ya 22 ndipo tena amerejea kileleni, sasa akiwa ni Makamu wa Kwanza Rais wa Zainzibar, lakini akitokea Chama Cha Wananchi CUF.

Kisiasa, Maalim Seif amepitia katika nafasi nyingi sana. Mwaka 1977 – 1988 alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM lakini pia mwaka 1977 – 1987 alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM huku mwaka 1982 – 1987 akiteuliwa kuongoza Idara ya Uchumi na Mipango ya Chama cha Mapinduzi (kitaifa).

Maalim Seif na wenzake kadhaa walifukuzwa kutoka Chama Cha Mapinduzi mwaka 1988 baada ya kushindana kimsimamo na CCM na alikuwa mmoja wa waanzilishi wa vuguvugu la “Kamahuru” la Zanzibar lililoungana na CCW (Chama Cha Wananchi) ya Tanzania Bara na kuunda Chama Cha Wananchi CUF ambapo yeye (Maalim Seif) alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa CUF akihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1999 alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CUF hadi hivi sasa.

Kimataifa, Maalim amewahi kushikilia wadhifa mkubwa sana kimataifa kati ya mwaka 1997 – 2001, alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa “The Unrepresented Nations and Peoples Organization (UNPO)” (Nchi zisizowakilishwa na Mashirika ya Watu) – Tafsiri yangu. Hii ni taasisi ambayo makao makuu yake yapo jijini The Hague nchini Uholanzi na inahusisha mataifa zaidi ya 50 duniani na watu ambao siyo wajumbe wa Umoja wa Mataifa, yaani ambao wakienda Umoja wa Mataifa wanakuwa na hadhi ya waangalizi tu (au wageni). Baadhi ya nchi mwanachama wa umoja huu ni pamoja na Taiwan, Tibet na Zanzibar. Lakini pia amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Vyama vya Kiliberali Duniani kati ya mwaka 2002 – 2003.

Maalim Seif amemuoa Aweina Sinani Masoud tangu mwaka 1977 na wana watoto watatu.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s