Rushwa haivumiliki- Jahazi Asilia

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Jahazi Asilia Bw Kassim Bakar Ali (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana, kuliani mwake ni Makamo wa rais wa chama hicho Bw Jumanne Pembe Kinyogori, na kushoto ni katibu mkuu wa chama ni Mtumweni Jabir Seif
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Jahazi Asilia, Kassim Bakar Ali (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana, kuliani mwake ni Makamo wa rais wa chama hicho, Jumanne Pembe Kinyogori, na kushoto ni katibu mkuu wa chama ni Mtumweni Jabir Seif

Salma Said

Mwenyekiti wa Chama cha Jahazi Asilia, Kassim Bakar Ali ametangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar huku akiahidi kupambana na rushwa iliyokithiri katika taasisi nyingi za serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa watu wenye ulemavu Zanzibar, Ali alisema ni dhambi kubwa sana kula mali ya umma hivyo chini ya uongozi wake kipaumbele ni kupambana na wale wote wenye kufanya ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na wenye kupokea rushwa.

 

“ lazima kuwepo na usimamizi wa fedha za umma kwa sababu hizo ndio zinazoendeshea serikali na kuleta maendeleo lakini wakiachiwa watu wafuje na waziibe ovyo serikali itakosa fedha za kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa hivyo mimi chini ya uongozi wangu siwezi kukubali vitendo hivyo kabisa” aliahidi Mgombea huyo.

 

Aliwaambia waandishi wa habari wakati anatangaza nia lakini tayari chama chake kimeshatoa fomu na amesharudisha na anasubiri Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itangaze ili wafuasi wake wampeleke kuchukua fomu ili kusubiri kampeni na kushinda katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Octoba mwaka huu.

Mwenyekiti huyo amesema ipo haja ya kutengenezwa mazingira mazuri ya ushindi kwa wote na badala ya mfumo uliopo sasa ambao mara nyingi chama cha mapinduzi ndio kinachoshinda na kuchukua kila kitu na wengine wanapewa kama zawadi.

 

”Wakati wa uchaguzi uliopita Maalim Seif alisema ushindi huu ni wa wazanzibari wote na sio wa chama kimoja tu basi kauli ile ni nzuri na tunataka tuwe na ushindi wetu sote na sio chama kimoja tu cha CCM”aliongeza.

Chama cha Jahazi Asilia kiliasisiwa na Kaka wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Abuubakar Amour Juma (Marehemu) kimepata wafuasi wengi kutoka Kaskazini Unguja ambapo anatokea Rais Mstaafu Dk Salmin Amour Juma.

 

Akizungumzia madhumuni ya chama hicho kuchukua fomu ya kuwania urais, Mwenyekiti huyo amesema ni kutumikia wananchi kwa kushirikiana bila ya ubaguzi, kueneza elimu ya uraia na kujua haki na wajibu kwa kila mwananchi kama inavyobainishwa kwenye waraka wa umoja wa mataifa katika kutambua dhamana na wajibu wake.

 

Mgombea huyo amesema mwenendo wa uamuzi na utekelezaji wa chama hicho utakuwa katika msingi wa makubaliano ya wote wala sio kwa msingi wa wengi  kulingana na Imani ambapo demokrasia ya kweli ni kuepuka wengi kutawala na kuwaacha wachache.

 

Aidha chama hicho kimesema kinaungana dhana ya serikali ya umoja wa kitaifa na kuepukana na mifarakano lakini wanataka mfumo huu uliopo sasa ubadilishwe kwani hauonekani kama ni serikali ya umoja kwa kuwa umeshirikisha vyama viwili vya CCM na CUF  na sio vyama vyote vya kisiasa nchini.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s