Nitawaachiwa wananchi kujiamulia- Karume

Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Nia hiyo aliitangaza katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya kati uliopo Dunga Zanzibar.
Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Nia hiyo aliitangaza katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya kati uliopo Dunga Zanzibar.

Salma Said

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Ali Karume ametangaza nia ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku kipaumbele chake kikiwa ni kutoa uhuru wa aina tatu kwa wananchi wote.
Akizungumza katika hafka hiyo iliyoambatana na shamra shamra za kutangaza nia iliyofanyika Dunga wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja Balozi Karume amesema lengo lake ni kuwania nafasi hiyo ili kupokezana kijiti na kuendeleza yale yaliotangulizwa na chama chake.
Akizungumzia kipaumbele chako cha kwanza Karume amesema suala uhuru lipo kwa namna tatu ambapo alisema kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa kujiamulia ikiwa chama cha siasa au dini aitakayo au jambo lolote ambalo linakubalika katika sheria za Tanzania.
Akizungumzia suala hilo hilo la uhuru alisema pia kuna uhuru wa kujituma na kutaka kufanya biashara lakini anawekewa vikwazo vya kila namna katika nchi yake.
“Uhuru wa kujituma ni muhimu sana kwa kila mtu sio mtu anataka kuunza njugu wewe unamwambia huna leseni…lesini kwani anataka kuendesha gari mtu akitaka kuendesha gari ndio mdai leseni lakini sio kuuza njgu lazima watu wapewe uhuru wa kujituma” alisema Karume.

Karume alisema kuna pia uhuru wa kuepukana na njaa ambapo huo unatakiwa kuanzishwa viwanda ili kuzindika mazao na bidhaa mbali mbali nchini.

Karume alitumia mua mwingi kuelezea historia ya nchi na chama cha mapinduzi ilipotoka ambapo alisema ni muhimu kwa wanachama hao kuwachagua viongozi wenye uelewa mzuri wa kimataifa na sio watu ambao wanashindikiza na kutia aibu mbele ya mabalozi wa nchi za nje.
“Hatutaki mtu wa okay, sir au yes sir tunataka mgombea ambaye anaelewa mambo ya kidiplomasia na anajua kuzungumza na mataifa mbali mbali sio anakwenda ulaya anashindwa kuongea badala yake anaitikia tu yes sir” amesema.

Hata hivyo amewataka wanachama hao kuwachagua viongozi kwa vigezo vya uwezo na uadilifu na sio kuwa wamekaa muda gani katika matawi na mashina ya chama huku akisisitiza mgombea  asichaguliwe kwa kigezo cha uzanzibari wake au utanganyika wake jambo ambalo limekuwa likiwakoseshwa wengine haki ya kuingia katika kinyanganyiro hicho kutokana na khofu za kutopita.

 

Balozi Karume aliwapiga vijembe wagombea wenzake waliotangulia kutangaza nia kwa kusema ingawa wapo wagombea ambao tayari wameshatangaza nia lakini wanachama wawe makini kuwachagua kwa kuwa wapo ambao tayari wameshawahi kuwepo katika uongozi wa wakaharibu.

“Wapo watu wamekuwepo na tumewaona wameizamisha meli ndogo lakini sasa wanakuja kutaka tuwape watuendeshee meli kubwa wakati tunawajua sasa tunakwambieni msije mkakubali na sisi wengine tunakaa kimya lakini wakija tunasema hapana wewe uliizamisha meli ndogo wewee na tutasema huyu anayetaka kuiongoza jamhuri ndio yuleee” alisema huku akipigiwa makofi.

Karume alitumia muda mwingi kutoa mifano historia ya chama kilipotoka, uzoefu wake wa kuishi nchi za ughaibuni huku akijisifu kuwa amesoma na ni mwana uchumi na kuwaponda wana uchumi wenzake wa Tanzania ambao wamekuwa wakisema dola imeshuka.
“wapo watu waliosema kuwa wamefanya maamuzi mazito lakini na sisi wengine tunasema tutafanya maamuzi mazito hivyo hivyo”.
Aidha aliwapiga vijembe wenzake waliotangulia alisema wapo baadhi ya wagombea ambao wametangaza anataka kuunda Tanzania mpya jambo ambalo alisema haliwezekani kwani Tanznaia ni hiyo hiyo na haiwezi kuwa nyengine.
Alisema wapo watu waliosema hawatakubali kilimo kwanza na watawekeza kwenye elimu, ambapo amesema hata yeye atawekeza kwenye elimu lakini na suala la kilimo ni muhimu sana katika nchi kwani historia ya nchi hii inatokana na kilimo na amesema ataweka atatoa umuhimu Zaidi katika suala la uchumi.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s