Hamad Rashid: Mbunge wa Jimbo la Wawi

Hamad Rashid Mohammed
                Hamad Rashid Mohammed aliyetangaza nia ya kuwania urais wa Zanzibar 

Historia yake

Hamad Rashid Mohammed ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha wananchi wa Jimbo la Wawi, Pemba. Alizaliwa Machi Mosi, 1950 huko Zanzibar na kusoma katika shule ya msingi ya wavulana ya Chake kati ya mwaka 1958 hadi 1967. Amesoma Sekondari (kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1968–1970 katika Shule ya Sekondari Chanjamjawiri huko huko Zanzibar (Mzunguko wa Kwanza).

Hamad Rashid alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Fidel Castro kati ya mwaka 1970–1971. Na wakati huohuo kati ya mwaka 1974–1976, alipata mafunzo ya muda mrefu ya masuala ya Kibenki katika Chuo cha Mafunzo cha Benki ya NBC.

Baadaye mwaka 1980 Hamad Rashid alijiunga katika chuo cha Itikadi cha Zanzibar na kupata stashahada kati ya mwaka 1981 na mwaka 1981 alienda kusoma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis Xavier kilichoko huko Antigonish katika mji wa Nova Scotia nchini Canada, na kuhitimu stashahada ya Maendeleo ya Jamii mwaka 1982.

Kwa upande wa ajira, Kwa miaka mitano (1972–1977), Hamad Rashid aliajiriwa na Benki ya Watu (People’s Bank) kama karani na mwaka 1979 hadi 1982 akateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Ushirika Tanzania.

Kisiasa, Hamad Rashid amekuwa mwanachama wa ASP na baadaye CCM, kabla hajahamia Chama Cha Wananchi (CUF) baada ya kufukuzwa CCM mwaka 1988. Amekuwa Katibu wa Vijana wa ASP kati ya mwaka 1970-1972, amefanya kazi na benki ya ASP kati ya mwaka 1972 hadi 1977, amekuwa mwakilishi wa CCM katika Chama Cha Ushirika kati ya mwaka 1978–1988 na amewahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuanzia mwaka 1982-1988.

Uanachama wa Hamad Rashid na wenzake kadhaa ndani ya CCM ulikoma mwaka 1988 baada ya chama hicho kuwavua nyadhifa zao zote za uongozi wa kichama na kiserikali kwa sababu ya tuhuma kadha wa kadha ambazo ni vigumu kuzithibitisha hadi sasa. Yeye mwenyewe na wenzake mara kadhaa wamesisitiza kuwa walifukuzwa kwa kuonewa na kwa sababu tu walionekana wanatetea misimamo thabiti ambayo CCM haikuipenda kwa woga usio na maana.

Mwaka 1992 Hamad Rashid alikuwa mmoja wa waasisi na waanzilishi wa Chama Cha CUF ambako ametumikia nyadhifa kadhaa za ndani ya chama ikiwamo ukurugenzi wa chama katika vipindi kadhaa, ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa na Ujumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa.

Hamad Rashid akiwa CUF alikuwa mmoja wa viongozi waliofanya kazi kubwa katika kusimamia mazungumzo ya kutafuta muafaka kati ya CUF na CCM (akiiwakilisha CUF).

Hamad Rashid ameoa na ana watoto.

Mbio za ubunge

Akiwa ndani ya CCM, Hamad Rashid ni mmoja wa wanasiasa walioanza kuwa wabunge takribani miongo zaidi ya mitatu iliyopita. Amekuwa mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 1978-1988 na wakati huo pia akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania kati ya mwaka 1980–1982 na Naibu Waziri wa Madini, Fedha na Uchumi wa Tanzania kati ya mwaka 1982–1988.

Chanzo: Mwananchi

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s