Soma gazeti lako An-Nuur Ijumaa

annuurSoma nakala yako hapa: –

One Reply to “Soma gazeti lako An-Nuur Ijumaa”

  1. Nikiwa Mmoja wa wafatiliaji wa Kampeni za Mbunge wa Monduli Mr. E. Lowassa ; Tunamuona akijipendekeza hivi sasa kwa waislaam aidha kwa maneno yake au kwa michango yake kwa hao waislaam …hakuna asiejua kuwa ni mtu wa karibu sana na Rais Kikwete , na wengi wetu tunaelewa na kuamini kwamba CCM chini ya mwenyekiti wake watampitisha Bwana huyu kugombea urais kwa tiketi ya chama cha CCM ktk Uchaguzi unaokaribia . Lakini wengi ya watu na hasa waislaam hawajamuelewa ni nani Bwana Lowassa na ipi mikakati yake ya utawala , na yeye ni mtu wa kikundi gani au akina nani wapo nyuma yake ….
    Napenda kuchukua fursa hii kwa kuwatahadharisha waislaam na watanzania wenzangu kwa ujumla , kuhusu maovu aliyoyafanya bwana Lowassa kwanza kwa kujikumbusha TUHUMA mbali mbali za wizi wa mali ya umma na pato la serikali zilizowashirikisha waheshimiwa wengine akiwemo yeye Bwana Lowassa na Partner wake mkubwa Bwana Rostam Azizi ambaye hivi sasa anaishi nje ya nchi baada ya kukimbia na Mabilioni ya Dollars …hawa ni watu hatari kabisa ktk nchi yetu ambao wameifisidi serikali yetu na hivi sasa wanataka tena wachukue madaraka ya juu kuimaliza nchi yetu hii .
    Ama kwa upande wa Waislaam , wanatakiwa wamuelewe Bwana Lowassa amejiiimaarisha sana kuyarubuni baadhi ya magazeti nchini na vyombo vya habari kwa kutumia zile hela na hela anazotumiwa na Partner wake Bwana Rostam Aziz kwa lengo la kufanya kampeni zake hizo ambazo sote tunajua na tunaona kwa macho MAHELA mengi yanatumika safari hii ktk kampeni za uchaguzi huu. Bwana Lowassa anajua umuhimu wa kampeni zake kwa kutumia MEDIA channels , ili apate kujisafisha na kuwa karibu na watu kwa kuvaa gozi la kondooo kumbe ni chui aliejifisha !
    Bila shaka hela zake hazikuishia kwa hao editors wa magazeti bali zimewafikia hata wakuu wa makanisa makubwa ya hapa nchini ….ndio maana Makanisa yanampigia debe sana Bwana Lowassa -na kwao ni mtu mwema na mfuasi mzuri atakayekuja kuyatekeleza yale yale aliyoyafanya Bwana Mkapa wakati wa utawala wake na ahadi nyengine nyingi zitakazowapendezesha wakuu wa makanisa nchini .
    Huyu Bwana ameshachukua kiapo na ahadi nyingi kwa hao wakuu wa makanisa , na bila shaka Ahadi zake ataziitekeleza akiwepo madarakani. Jambo la kuhuzunisha na kusikitisha kuwaona waislaam wanavyonunuliwa kirahisi na huyu Bwana -Hela ndogo za Milioni walizopewa Msikiti wa Mtambani amabzo zilikuwa ni mchango wa kusaidia ujenzi wa shule ilioungua ….Masheikh wakamuona Lowassa ni mtu wao na akaanza kusifiwa hata kwenye khotba za Ijumaa . na hivi kwenye kampeni zake huwapelekea vihela vichache kwa masheikh kama tunavyoona hali ilivyo huko Arusha , Masheikh hawa hupokea hela hizo kwa ajili ya mambo ya dini bila ya kuhoji uhalali wa hela za Lowassa zinatoka wapi na amezipata wapi ? na je! hela kama hizo zinafaa kutumika kwa shughuli za dini ?

    Gazeti letu la ANNUUR nalo limesharubuniwa na kunaswa ktk kampeni za Lowasssa kwani tunashuhudua hivi sasa maelezo yake na picha zake zikitokea ktk “HEADLINES” … Aliekuwa muovu juzi leo anasifiwa kuwa mwema !

    WAISLAAM WA TANZANIA WATAENDELEA KUWA WATUMWA NA WANYONGE KTK NCHI YAO WENYEWE NA WWTAENDELEA KUTUMILIWA NA MFUMO KRISTO IKIWA BADO WAMEWEKA MASLAHI YA DUNIYA YAO MBELE KULIKO MASLAHI YA DINI YAO .BADO TAASISI ZETU NA MASHEIKH ZETU ZINAENDELEA KURUBUNIWA NA HAO HAO MAADUI WA KIISLAAM ..KWA THAMANI NDOGO TU YA KIDUNIA ….JE TUTAKWENDA KUMJIBU NINI MOLA WETU SIKU YA MALIPO ?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s