Sheikh Farid wa uamsho aibua mapya mahakamani

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed
Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed

Dar es Salaam. Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) anayekabiliwa na kesi ya ugaidi na wenzake 23, wa Jumuiya ya Uamsho, wamesema wanahitaji Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Katiba wa Zanzibar, waende gerezani kuonana nao.

“Tunaomba iwe ndani ya siku saba, zikiisha uamuzi tutakaoutoa tusije kulaumiana, hatuwezi kudhulumiwa haki yetu tukakaa kimya,” alidai Sheikh Farid jana muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Janeth Kitali kudai mbele ya Hakimu Mkazi, Renatus Rutta kuwa kesi yao ilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Kitali alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na pia bado wanasubiri kumbukumbu za Mahakama Kuu ili waweze kupeleka rufaa yao katika Mahakama ya Rufani.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Sheikh Farid alidai kuwa kesi ya ugaidi inayowakabili ni ya bandia na madai yao yalikuwa ni kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka yake sahihi na Muungano hawautaki na kwamba, madai hayo ndiyo yaliyosababisha wao kupata misukosuko na kujikuta wakibambikiwa kesi ya ugaidi.

Alidai kuwa katika kesi hiyo, wapo washtakiwa ambao wamegoma kula na wanne kati yao wana hali mbaya kiasi cha kuwekwa katika eneo maalumu. Aliiomba mahakama ikawaangalie au isubiri kupokea maiti ili iingie kwenye Historia ya Zanzibar.

Hakimu Rutta alipokea taarifa hiyo, alimhoji askari magereza kama kweli mahabusu hao wamegoma kula, naye alikiri na kudai kuwa wamegoma hata kufika mahakamani.

Lakini mshtakiwa Salum Ally alikanusha kauli hiyo ya askari magereza na kudai kuwa hawakugoma kufika mahakamani bali walishindwa kwa sababu ya kukosa nguvu.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Rutta alisema ni haki ya watu waliopo gerezani kutembelewa na wanapaswa kutendewa kwa kadiri inavyopaswa.

Alimweleza Sheikh Farida na wenzake wakawaeleze wenzao kuwa wanapaswa kufika mahakamani na madai yao yatafanyiwa kazi.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, uliotolewa na Jaji Fauz Twaib ulioamuru Mahakama ya Kisutu kusikiliza na kutolea uamuzi hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi

Upande wa utetezi katika hoja zao, walikuwa wakiiomba mahakama ya Kisutu ifute mashtaka ya ugaidi dhidi yao, pia walihoji uhalali wa kushtakiwa Tanzania Bara wakati Zanzibar ni nchi ambayo ina Mahakama Kuu na kuomba wakashtakiwe katika sehemu walizokamatwa.

Katika kesi hiyo, Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye pia ni kiongozi wa jumuiya hizo na wenzake wanakabiliwa na makosa manne ya ugaidi.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s