Dk Shein afanya mabadiliko ya wilaya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein

Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya mipaka katika baadhi ya mikoa na wilaya, huku akizindua upya shehia 384 za Unguja na Pemba.

Mabadiliko hayo yanatoa mwelekeo wa mipaka ya majimbo yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilika kazi hiyo.

Dk Shein amefanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Ibara ya 2A na Kifungu cha Nne cha Sheria ya Tawala za Mikoa namba nane ya mwaka 2014.

Pia ameridhia kuweka upya mipaka ya wadi ili kukidhi mahitaji ya idadi ya watu.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, Haji Omar Kheir ilisema Zanzibar itaendelea kuwa na mikoa mitano, unguja mitatu na Pemba miwili.

Ilisema mipaka ya mikoa miwili ya Pemba itakuwa na mabadiliko kwa kuzihamisha Shehia za Ole na Mjini Ole kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenda Kusini Pemba.

“Kutakuwa na Wilaya 11 badala ya 10, baada ya ile ya Magharibi kugawanywa kuwa mbili ambazo ni Magharibi A na Magharibi B,” ilieleza taarifa hiyo.

Wilaya ndogo za Tumbatu na Kojani zitaendelea kufuata mipaka ya awali, isipokuwa baadhi ya shehia zimehamishiwa katika wilaya nyingine, zikiwamo za Kipange, Muwanda na Mchangani ambazo zitakuwa Kaskazini A kutoka Kaskazini B. Shehia ya Kisogoni imehamishiwa Kaskazini B kutoka Kaskazini A.

Taarifa ilieleza kuwa shehia nyingine zilizohamishwa ni Michamvi ambayo itakuwa katika Wilaya ya Kusini badala ya Kati na Shehia ya Pete imehamishiwa Kati kutoka Kusini Unguja.

Nyingine ni shehia za Finya, Kinyasini na Mgogoni ambazo zimehamishiwa Wilaya ya Wete kutoka Micheweni. Shehia ya Dodo imehamishiwa Mkoani kutoka Wilaya ya Chakechake, Pemba. Mkurugenzi wa ZEC, Salum Kassim Ali alisema jukumu la Rais wa Zanzibar kukata mipaka limeshafanyika, hivyo wanaendelea na mchakato wa kutayarisha majimbo mapya ya uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “Dk Shein afanya mabadiliko ya wilaya”

  1. Asalam alaykum kwa ukweli kwa Maoni yangu bajet ni nzuri ikiwa yatatekelezwa Yale Yalio orodheshwa kwa kiasi Fulani itawasaidia wazanzibar ila Ina upungufu Mkubwa kwa kuwa Bado tegemezi saana viashiria tu vya mapato Bado hakuna mikakati kamilifu ya vyanzo vya mapato mengi ninayo ila naiunga mkono kwa Asilimia 40

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s