Vitimbi vya CCM hawana mpya imepoteza dira na sifa za kuongoza

Dk Salmin Amour Juma (Komandoo)
Dk Salmin Amour Juma (Komandoo)

Wakati vyama vingi vinaanzishwa tena hapa Zanzibar vilianza na matumaini makubwa kutoka kwa wananchi baada ya kuchoshwa na ukiritimba wa chama kimoja. Matumaini makubwa yalitegemewa kupatikana kutokana na “chama tawala” kwamba kilikuwa tayari kujisahihisha na makosa yao ya nyuma na kutandika na kuonyesha njia na mwelekeo mpya wa kuongoza Taifa badala ya uchu wa kutawala.

Sababu zozote zile naziwe katika kuleta na hatimae kukubali mfumo wa vyama vingi mategemeo ya mabadiliko yalitarajiwa kuwepo na kuwepo kwa kiwango kikubwa pamoja na kusahau yaliyopita, ijapokuwa wengi walioathirika wamesamehe lakini hawakusahau.

Hali haikuwa hivyo bali ilikuwa kunyume chake ,chuki ,ubagizi ulizidi kushamiri na kupaliliwa. Miaka ishirini na tatu katika uhai wa taifa ni kidogo mno, ni kama jana au juzi tu ilipoanza enzi ya Dr. Salmini bin Amour “Komandoo” baba wa upandikizi fitna, chuki na ubaguzi baaina ya wapemba na waunguja kwa sababu tu Wapemba wamekikataa Chama cha Mapinduzi.

Salmin Amour aliwaondoa Wapemba wote katika nafasi za uongozi katika serikali alimbakisha Shajak tu. CCM ilianza kuwabagua na inaendelea kuwabagua wazanzibari na kuwaweka katika mafungu na madaraja.

Hawa ni waswahili na hawa ni waarabu, hawa ni wapemba na hawa ni waunguja, hawa ni weupe na hawa ni weusi, hawa ni wazanzibari halisi na hawa si wazanzibari halisi, hawa ni wenzetu na hawa si wenzetu. Imekuwa ikitumia misingi ya makundi iliyoyajenga na kutunga lugha za kibaguzi kwa kundi moja dhidi ya jengine. Imekuwa ikitoa ajira kwa upendeleo kwa msingi wa makundi hayo.

Imekuwa ikitoa huduma za kijamii kwa upendeleo pia kwa msingi wa makundi hayo. Imekuwa ikitoa nafasi za vyeo serikalini kwa upendeleo (sote tumeisikia clip ya Waziri wa Tawala za Mikoa Haji Omar Kheri ya kibaguzi).

Mwakilishi wa Tumbatu Haji Omar Kheri
Mwakilishi wa Tumbatu Haji Omar Kheri

Hiyo ndio CCM. Mpaka leo CCM imekuwa ikifanya unyanyasaji na mateso kadhaa wa kadhaa hata ya kisaikologia kwa msingi wa makundi hayo. Kufanya wengine ni wenye nchi na wengine ni wahamiaji tu .Nani aliesahau kauli ya Komandoo katika mkutano wa kibanda maiti akijitutumua kwa kusema “Wapemba weshasoma sasa zamu ya wenzao Waunguja”, kauli iliyomfanya Shamhuna waziri wa Mipango kufunga njuga na kuwanyima Wapemba nafasi za Masomo ndani na nje.

Hivo nani kasahau kauli ya Rais Ali Hassan Mwinyi aliposema “hawa wapemba ni vijibwa vya santuri wanaiga sauti za mabwana zao” yaani leo wapemba si watu na wapemba hawana haki ya kutoa mawazo yao?.

Kauli nyingi za dharau na kejeli zilitolewa hata kufika hadi kusemwa Mpemba kuingia Ikulu ni sawa na mbwa kuingia msikitini.CCM kama kingalikuwa ni ‘chama cha kuongoza nchi’ sio kutawala basi kingefanya utafiti wa kina kujua sababu ya Wapemba kuikataa CCM ili kufahamu lakini CCM ni “chama cha kutawala” hata bila ya kupata ridhaa ya wananchi, lakini maskini ni chama ambacho kimeshapoteza dira na mwelekeo haya yalisemwa zamani na aliekuwa Katibu Mkuu CCM Kolimba hivi sasa inathibitika wazi kuwa yale yaliosemwa yalikuwa ni sahih.

Vyama vingi vilianza kwa vishindo, vishindo ambavyo vilidhamiria kuleta maendeleo na mageuzi ya kiuchumi na kijamii kinyume chake CCM kilikuwa na azma ya kuzima harakati za vyama na vugu vugu la kutaka mabadiliko.

Vishindo hivyo vya CCM vilitumia nguvu za dola bila hata kujali Katiba wala sheria za nchi.Vyama vya siasa ambavyo viliruhusiwa kufungua matawi pamoja na kufanya mikutano ili kuweza kunadi sera zao na kuweza kukubalika hii ikiwa ni haki yao chini ya sheria, lakini haikuwa hivyo pale chama cha CUF kilipofungua tawi na kuperushwa bendera Shumba Mjini (Pemba) ndipo alitokea Mkuu wa wilaya Feruzi na kupeleka askari wa FFU ilikuteremsha bendera ya chama cha CUF, nguvu za kupita mpaka zilitumika na jeshi la polisi lilitumika na walitumia risasi na kuua pamoja na kujeruhi.Nani amesahau mauaji ya kijana Awadh hapo Mtendeni.

Hili linajirudia kwa mikakati ya shari za Haji Omar Kheri katika mikakati yake ya shari huko Tumbatu kwa kupanga njama. Hatuzi kusahau watu waliouawa katika maandamano ya amani kupinga mtokeo ya uchaguzi yaliyofanya CUF. Wengi walijeruhiwa na kuwa na vilema vya maisha na wengine kukimbilia Kenya baada kusakwa kwa mabunduki kama nguruve, nini wameandamana .

Sote tunakumbuka pale Maaalim Seif pamoja na viongozi wenzake wa CUF akina Juma Duni, Maulid Makame, Mloo na wengineo walifunguliwa kesi (za nyaraka za siri, uchochezi na uhaini) ili kuzuia na kuwafumba midomo katika kuikosoa CMM na kutokubaliana na sera za CCM. Sasa hii leo si ajabu kuona kesi inayomkabili Mansour baada ya kuikosoa CCM na sera zake kwa Zanzibar za kuendeleza ukoloni wake.

Tumethibitishiwa na Malenga wa Matusi Borafya katika mkutano wa hadhara kuwa kesi ya Mansour ni ya CCM,pale alipomtaka Raisi aishughulikie Kesi ‘kesi yetu ya Mansour”Hii ni ile ile siasa za kutisha na kuwatia khofu wananchi na kuwanyima uhuru wa maoni wananchi. Hivo Mansour hiyo silah kaipata leo na hizo risasi kapewa na CUF?.

Nani asiejua kwamba Mashekh wa uamsho wameonewa na kupandikiziwa kesi kwa kutoa maoni yao kuhusu Muungano. Hivo huko bara Mapadri hawatoi maoni kuhusu muungano, au wana CCM hawatoi maoni yao kuhsu muungano ,mbona wanao fungwa au kufukuzwa chama kwa kutoa mawazo ni Wazanzibari tu. Kila leo vigogo wa CCM wanaikosoa na kutoa maoni yao lakini hatujasikia kufukuzwa.

Katika miaka ya mwanzo ya kuanzishwa au kurudishwa tena mfumo wa vyama vingi viriri vya mikutano ya siasa vilishamiri kwa matusi ya akina Omar Awesu na Aley marzuku wakati ule hii leo tunaona si jambo la ajabu kumuona malenga wa matusi Borafia akijilabu kwa kutukana watu bila hata kuheshimu mila na utamaduni wa Kizanzibari na bila ya kukemewa.

Kwa upande mwengine Viongozi wa chama na serikali walikuwa mstari wa mbele kutunisha misuli yao na kutumia vyombo vya dola, Mkuu wa mkoa Kaskazini Unguja wakati ule Abdulla Rashid alitumia nafasi yake kukataza na kuzuia mikutano ya CUF kutofanywa katika mkoa wa Kaskazini na kuwazuia viongozi wa CUF kutokwenda Kaskazini.

Bila kujali haki za kikatiba za uhuru wa mtu kwenda atakako na haki ya kisheria ya kufanya mikutano, Si ajabu kusikia Mkuu wa Mkoa Kaskazini Tindwa kuchukua hatua kama hiyo kwani kama kawaida yao Polisi kama vyombo vyengine vya dola hujiingiza kichwa kichwa katika siasa, leo Mkuu wa Polisi anakataza kufanyika kwa mikutano ya kisiasa katika sehemu moja ya nchi.

Hii ni kinyume na sheria Polisi haina haki hii , kazi yao ni kulinda usalama na sio kuratibu shughuli za kisiasa. Abdalla Rashid huyu huyu alipokuwa Mkuu wa Mkoa Mjini aliongoza kuvunja nyumba za Wapemba Mtoni na bububu.

Yale yale ambayo aliyokuwa akiyaratibu Mheshimiwa Raza ya kuwapa mipira timu za mipira ili kuzuia viwanja visiweze kutumika kwa mikutano yanajirudia tena katika siku hizi za karibuni, kumekuwa na kuzuiliwa mkutano kwa kisingizio ati wenye kiwanja cha mpira au sehemu umma “public ground” haitotumika kwasababu watu wanataka kucheza ngoma au mpira haya yalikuwa yakiratibiwa na Raza

Mohammed Raza
              Mohammed Raza

na kuwahusisha Polisi. Raza alifika hata kugawa mpanga katika maskani. Hatumlaumu Raza kwa kutoa TV kwa maskani lakini kutoa mapanga, hili anapaswa kulaumiwa.

Matokeo mabaya ya kushambuliwa wanachama wa CUF wanapokuwa katika safari za kurudi mikutanoni yalikuwa yakitoa mara kwa mara hasa kwa upande wa kaskazini hapo miaka ya nyuma leo hii tena matokeo ya kushambul;iwa wanachama na wapenzi wa CUF yanajirudia tena. Hivi karibuni mashambulizi mabaya sana yamewakumba wanachama na wapenzi wa CUF mara hii walipokuwa wanarudi mkutanoni Makunduchi.

Vitimbi hivi vya CCM ni vingi na si vigeni katika siasa za Zanzibar ,ubao wa Kisongo umekuwa ukitumika tokea enzi kuchochea fitna ,chuki na mgawanyiko, Leo kisonge inatamka Wapemba wende kwao, Wapemba wahame, Wapemba na warabu wahame, unguja tumepindua. Hivo hizi zote siasa au ni kuishiwa.

Kufukuza kiongozi kama Hassan Nassor Moyo na wengine waliofukuzwa kabla yake inaonyeza wazi kwamba meli inakwenda mrama na kufilisika kisiasa na kutovumilia na kuheshimu mawazo ya wengine. CCM inataka watu wote waimbe wimbo huo huo mmoja..

Mzee Hassan Nassor Moyo
Mzee Hassan Nassor Moyo

Ikiwa sera hizo sera za kibaguzi na kutokubali kusikia na kuvumilia mawazo tofauti bado hazitoshi CCM imepoteza matumaini kwa watu wa rika zote na hasa vijama pale inapo endelea kujinadi kuwa “chama”kwanza na kuisaliti nchi na wananchi wake na kuwa dalali wa Zanzibar kwa hata yale mamlaka yaliyobaki ambapo kama sio Chama cha CUF yangekuwa yameshakwenda na maji au arijojo.

Dk Ali Mohammed Shein Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar
Dk Ali Mohammed Shein Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar

CCM inaonekakana kuwa imeamua kuendelea kufanya udalali, kuiuza nchi kwa maslahi binafsi na tamaa na kutumia ubaguzi kwa kauli na vitendo na kuwagawa wazanzibari kuwa ni turufu katika chaguzi.

Bado CCM iko katika usingizi wa manane na kuota ati mwarabu atarudi. Hivyo mwarabu gani ataerudi kutawala Zanzibar. Ikiwa mwarabu atarudi basi ni katika kuitikia maombi ya msaada unaoombwa na viongozi wa CCM na Serikali , leo Kikwete, kesho Makinda,akifatiwa naBenard Membe ,Lukuvi na akina Shamhuna na Dr. Makame wakibeba mikoba yao kuelekea arabuni.

Ipo siku utabiri huo utatimia, utatimia kwa namna gani, mimi sifahamu. Wapo waliojaribu kutoka CCM na kuanzisha vyama vyao au kujiunga na vyama vingine vya siasa vilivyopo, pengine mshindo wao haukuweza kuing’oa CCM, lakini ni makosa tukisema kuwa mshindo wao ulikuwa mdogo
Ipo siku utabiri huo utatimia, utatimia kwa namna gani, mimi sifahamu. Wapo waliojaribu kutoka CCM na kuanzisha vyama vyao au kujiunga na vyama vingine vya siasa vilivyopo, pengine mshindo wao haukuweza kuing’oa CCM, lakini ni makosa tukisema kuwa mshindo wao ulikuwa mdogo

Ndio hao hao akina Lukuvi wakirudi huku kuwalani warabu na kumpa chambi malenga wa matusi Borafya kutukana warabu. Chombo kimeshawashinda kinakwenda mrama nahodha Borafya. Viongozi na wanachama wao wachache waliobaki walioshibishwa chuki kwa thamani ya elfu mbili, kofia na fulana pamoja na tamaa za ajira, bado wanaendelea na kucheza kuimba nyimbo za kuwabagua wazanzibari kwa rangi zao, asili zao na rangi za ngozi zao na kujidhatiti bila woga kuwapachikia mabango katika vigingi vyao yanayobeba kauli za kibaguzi.

Wanachama wa Chadema wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa ushindi katika Uchaguzi Mkuu. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam jana
Wanachama wa Chadema wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa ushindi katika Uchaguzi Mkuu. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam 

CCM Inaendela kuwapiga mafungu wazanzibari ili wachukiane, wahasimiane na wapigane. Huku ndio kupoteza dira na kuishiwa kisiasa. Vijana wa leo ambao wana malengo ya kujikwamua na hali duni ya maisha na kiu ya kutaka mabadiliko na maendeleo hawawezi kucheza nyimbo ya mwarabu atarudi au nyimbo za kuwagawa na kuwatawala wanyonge walio wengi.

Hizi zimepitwa na wakati.Wale ambao wanafurahia nyimbo hizo za kibaguzi ni dhahiri kwa wao na wazee wao wanafaidika na wananufaika na kugawanywa huku. wengi wa watoto wa wakubwa wamepelekwa nje kusoma, wengi wa watoto wa wakubwa wamepewa nafasi na nyadhifa kubwa serikalini na huwaoni wakikata mauno katika mikutano wala kufunga kambi katika maskani. Hebu tazama kulia ,kushoto ,mbele na nyuma kuna mtoto wa mkubwa katika mkutano huo wa CCM. Maskini za mungu munawadanganya watoto wa kimasikini na kuwatia chuki ili wahasimiane.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Mjini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Borafya Silima
Mwenyekiti wa Wilaya ya Mjini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Borafya Silima

Tukumbuke vilipoanza vyama vingi Maalim Seif alisema katika moja ya mikutano yake tutaanzisha vyuo vikuu ,tutawapatia kazi watoto wetu nje. Mheshimiwa Mapuri alijibu haraka haraka kwa kusema “watoto wetu watafanywa watumwa arabuni” leo hii watoto wangapi wapo arabuni wanafanya kazi na kusaidia wazee wao na familia zao.

Jee ni vizuri watoto hawa leo wakawa wanatumiliwa na kupakiwa katika mikutano ya CCM au kukaa mabarazani na kula unga, bila kujali maslahi yao. Baada ya tamko la Maalim Seif Serika ya CCM mbio mbio ilikurupuka na kutunga sheria za Chuo kikuu na sheria ya wakala wa kazi nje ya nchi. Nini CCM imefanya katika maeneo huru ? labda kuleta wairani kuuza tungule za vibati. Tumepoteza ajira katika viwanda vidogo.vidogo sehemu ya maeneo huru.

Dk Omar Ali Juma
                             Dk Omar Ali Juma

Yote ni kukosa sera za maendeleo. Salimin alifeli na sera za maeneo huru kwa udhaifu wa roho kuchagua watu kwa misingi ya kujuana na urafiki na ukuruba.. Bado CCM mnataka kutawala pamoja na kupoteza dira na mwelekeo, hivo chama kinaongozwa na Borafiya, na akina waride . Inabidi CCM iwaombe radhi Wazanzibari kwa kuwafikisha hapa walipo kwani wameishiwa hawana sera. Mareheremu Dr. Omar Ali Juma alikuwa akimwambia Maalim Seif “huna sera Balahau” leo na tujiulize na tutathmini kauli ya Dr. Omar ni nani aliyekuwa hana sera.

Advertisements

2 Replies to “Vitimbi vya CCM hawana mpya imepoteza dira na sifa za kuongoza”

 1. sikilizeni nyie wapumbavu, munasema baba angu aliwatukana, nyie cuf ndio mulioanza kumtukana baba angu na kumpigia goma ya vibati na kumtusi, na kmtumia wafuasi wa cuf mabarabarani kumtukana. historia ya seif sharif. tunaijua sana kulikuko nyie munaojifanya mashihata.
  baba angu alikuwa akishiriki mpaka ushirikina aliokuwa akiufanya seif ili awe rais wakati marehem baba angu yupo tanga, na marehem baba ndio aliyekuwa akituma barua za kumfukuzishia jumbe akienda kenya kuzituma alipokuwa aktumwa na seif.
  baba angu alitoka tanga baada ya kufanya kazi kubwa ya kuriksi maisha yakealiyokuwa akitumwa na seif, baada ta seif kuwa waziri kiongozi alimwita znz na kumtupa mtaani na sisi tukawa tunalaa kwa sud yusuf mgeni ukumbini, baada baba angu kufanya kazi kubwa ya kumuangusha jumbe aliyetumwa na seif kufika znz alipelekwa polisi kuruti wakati alipokuwa tanga alikuwa na mshahara mzuri na marupurupu pamoja na nyumba
  znz tulianza kuangaika kwa kutafuta nyumba na kukosa na waliotukosesha nyumba ni marafii wa seif hao leo cuf.
  baba angu aliacha kazi baada ya watu waseif kuhamishwa kazi na kupelekwa mikoani bara. katika maisha yote seif akiwa jela marehem baba angu alkwa akichangi pesa za kulishwa familia ya seif.
  baada ya marafiki wa seif kuenda dubai na kuiba pesa na kumsngizia baba angu apo baba angu alijiweka mbali na wizi hao wa seif.
  baada ya seif kuachiwa baba angu alimwendea seif ili mambo yawe sawa ijulikane wizi hao walioiba michango kutoka uae. seif alimuhaidi marehem baba angu kuwa atawaita wote ili baba ajue ukweli kwan waliib pesa na kumpa chack fake na baadaye wakasema alizwe baba angu.
  seif hakuwaita jamaa zake hao wizi ambao alitimuliwa madarakani.

  isitishe marehem baba angu alifanya kazi nzuri kabla ya kamahuru, ambayo kongamano la kuomba vyama vingi kuanzishwa, jamaa wa seif walimuendea baba angu na kumwambia asitoe hutuba na akitoa litakalomfika hawamo naye. na hutuba aliyoitoa iliwapndeza wenge kuliko hao marafiki wa seif.
  na waliponda kamahuru wakamtoa yeye sio kitu. seif yote hakuyaona hayo wala hakumwita baba angu kuhusu pesa wapambe wake waliowaibia waarabu na kimsingiza yeye.

  baada ya kuhutubia kule dar, baadhi ya familia yetu waliokuwa wakifanya kazi na baba walimfata wakamwambia utafutuwa sababu ukamatwe. na alipokamatwa hakuna hata mbwa moja aliotwambia nyoko na sisi tukiwa wadogo 3 tu tuiishi na baba etu.
  mie binafsi nilienda kwa seif na mzee mmoja alnipeleka akitumia gari ya baba seif akinijibu eti ni rafiki yao polisi wakati baba angu analala madema. na waliokuwa wakija nyumbani kuzungumza siasa wote walitukimbia.

  baba alipelekwa bara huko ili akateswe lakini polisi walishangaa eti kesi ni magazeti tu wakaenda kusachi kwa jamaa zake dar na kuambia alete watu wamahukulie zamana.

  baada baba kurudi nilimsihi aachane na kina seif pamoja na yule jamaa aliyetusaidia kuendesha gari. ndipo alipoaanzisha cha na kushauri ccm ijirekebishe. baada ya cuf kuona mambo ndio hivyo cuf walipeleka pesa ili wamtimue baba. lakini katika chama chake alitia wanafunzi wake wawili ndio wakaja kumwambia tushakula pesa tukutimue. ndio akaenda dar akajiuzulu.

  hapo ccm wakaanza kumfata na kumuhadaa. baada ya kuingia ccm alikuwa akieleza kujirekebisha, lakini cuf ndio walioanza kumtuka,
  na matusi aliyotukana baba angu sio haya ya leo ya nguoni, ilikuwa ni vichekesho tu. CUF WALIANZA NA YEYE AKAMALIZIA KUWAJIBU. WACHENI UNAFIQ WENU NI SHIHATA.

  baada ya muelekeo wa kuwaekebisha ccm kwa faida ya znz hao ccm ndio wakamwta eti naye cuf.
  NA KAMA SIO TATIZO LA SEIF KUWA UBEBERU LEO ENGEKUWA RAIS ZAMANI WA ZNZ. nyie wenyewe tizameni ABOUD na baba angu nani alistahiki kupewa madraka kwa kazi aliyoifanya kwenye ccm?
  lakini baba angu kila mara alikuwa msimamo wake ni znz na maedeleo kwa znz lakini tu ccm hawakuwa na nia hiyo.
  baba angu alifika kugombana na ccm pale kisiwadui kwa kuwatetea wapemba na mie nipo pale.

  hata hiyo hati ya muungano aliyokujakuidai ni baba angu. cuf kazi yao ni kutumikisha tu. wote waoga ndio ukaona jusa peke yake. ndio msemaji kama kidume wale wengine wapemba kula kulatu wanafiq

  miaka ya 2000 cuf walituma wazee wawili nyumbani ili waje wamshashi baba arudi awe na cuf na kumwambia ccm wamekutupa, mzee mmoja kutoka pemba mmoja unguja yule mzee wa kingazija. marehem akasema hataki wala hamuaini tena seif na watu wake.

  hata bi awena alipatanishwa na baba. seif wakati upo maisara hana mke pale.

  seif alishindwa kumjibu baba kwa sababu kuna mabo memngi walifanya ili afanikiwe mpanga kupindua ng`ombe kwa ushirikina MOLA AMASAMEHE NA MAKOSA YAKE MZEE WANGU.

  WALOANZA KUTUKANA NI CUF LEO MATUSI YAMWAZIDI YAMEWAGEUKIA. WACHENI UNAFIQ
  UTETEENI ZNZ YETU.

  1. eti balahau (seif) una sera ,mumliona kubwa . nyie mumemwitamarehem dr. kidonge cha lami.

   hamjaliona hilo?

   marehe idrisa mumemwita ng`ombe.
   hamjaliona hilo?
   MATUSI MUMEANZA, nyie wacheni zenu.

   TUELEKEZE KUDAI CHI YETUNA TUELIMISHE WENGINE. ILI TU NA UMOJA
   SISI NI WAISLAM TUTIZAME MWISHO MWEMA WA MTU.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s