Red Cross watoa msaada wa viatu kwa waathirika wa mvua

Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania { RED CROSS } Bwana Shaaban Ali Iddi akikabidhi msaada wa Viatu Pair 90 kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d kwa ajili ya watoto wa familia zilizopata maafa ambao wapo Kambini  Skuli ya mwanakwerekwe “C” .
Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania { RED CROSS } Bwana Shaaban Ali Iddi akikabidhi msaada wa Viatu Pair 90 kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d kwa ajili ya watoto wa familia zilizopata maafa ambao wapo Kambini Skuli ya mwanakwerekwe “C”

Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania (Red Cross) kimekabidhi msaada wa viatu Pair 90 kwa ajili  ya watoto wa familia zilizowekwa Kambini  katika Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe “C” baada ya Nyumba zao kujaa maji ya mvua.

Msaada huo umefuatia Mvua za Masika zilizotokea usiku wa kuamkia Tarehe 3 Mei mwaka huu na kuleta maafa makubwa yaliyosababisha zaidi ya  Nyumba 700 kuathirika  ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi na kuzikosesha makaazi Familia zilizokuwa zikiishi katika nyumba hizo.

Ujumbe  wa Red Cross Mkoa wa Mjini Magharibi ukiongozwa na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho Bwana Shaaban Ali Iddi umekabidhiwa msaada huo kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar  ambae pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salim Moh’d hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bwana Shaaban Ali Iddi alisema Uongozi wa Red Cross ulifikia hatua ya kutoa msaada huo baada ya kugundua kwamba  idadi kubwa ya watu waliohifadhiwa kwenye kambi ya dharura ya Mwanakwerekwe “C” ni Watoto wadogo.

Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akiushukuru Uongozi wa Red Cross kwa misaada yao ya Kibinaadamu waliyotoa kwa ajili ya familia zilizopatwa na maafa wiki iliyopita.
Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akiushukuru Uongozi wa Red Cross kwa misaada yao ya Kibinaadamu waliyotoa kwa ajili ya familia zilizopatwa na maafa wiki iliyopita.

Alisema Red Cross imeguswa na tukio hilo la mafuriko hivyo licha ya juhudi wanazochukuwa za kutoa misaada mbali mbali ya huduma lakini pia ikawajibika kuongeza msaada huo wa Viatu ambao kwa kiasi kikubwa utawasaidia watoto hao.

Mwakilishi huyo wa Mkutano Mkuu wa Red Cross Taifa aliyaomba Mashirika na Taasisi nyengine za Kitaifa na Kimataifa kuendelea kuguswa na Tukio hilo na kutoa misaada kwa jukumu hilo si vyema ikaachiwa pekee Serikali Kuu.

Akipokea Msaada huo  Katibu wa Kamatio ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar ambae pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rsis wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d aliipongeza Red Cross kwa jitihada zake inazoendelea kuchukuwa katika kusaidia huduma za Kijamii.

Dr. Khalid alisema Viongozi na Wanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania muda wote wamekuwa karibu na Serikali hasa wakati yanapotokea matukio ya majanga na maafa.

Katibu huyo wa Kamati ya Taifa ya kukabiliana na Maafa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Red Cross kwa hatua yake hiyo ambayo itasaidia kupunguza machungu ya Watoto hao, wengi kati yao wamepoteza vitu vyao vyote zikiwemo nguo na hata madaftari ya Skuli.

Alisema Kambi ya dharura ya Mwanakwerekwe “ C “ hivi sasa ina zaidi ya watoto 74 walio chini ya umri wa miaka 14  wanaoendelea kuhifadhiwa ambao watafaidika na msaada huo wa viatu.

Asilimia kubwa ya Watoto hao waliopo Kambini wamepoteza Vitu vingi ikiwemo Madaftari ya Skuli, Nguo, Viatu na vitu vyengine muhimu wanavyotumia ambavyo vingi kati yao tayari Idara ya Maafa kupitia Taasisi na Mshirika hisani wameshapatiwa “. Alifafanua Da. Khalid Salum Mohammed

Pia  aliyashukuru na kuyapongeza Mashirika na Taasisi za Umma na hata zile Binafsi zilizojitolea kutoa misaada mbali mbali ya Kibinaadamu na kuziomba zisichoke kwa vile bado mahitaji zaidi kwa waathirika hao yanahitajika.

Kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania  Red Cross Bwana Shaaban Ali Iddi, Mjumbe wa Red Cross Mkoa Mjini Magharibi Bwana Mwinyi Khamis Hamad na Makamu Mwenyekiti wa Red Cross Tanzania Bwana Salum Juma.
Kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Red Cross Bwana Shaaban Ali Iddi, Mjumbe wa Red Cross Mkoa Mjini Magharibi Bwana Mwinyi Khamis Hamad na Makamu Mwenyekiti wa Red Cross Tanzania Bwana Salum Juma.

Katibu huyo wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar alieleza kwamba Serikali imeandaa mpango maalum wa  usafiri kwa watoto wote waliopo Kwenye Kambi ya dharura Mwanakwerekwe “C” kuendelea na masomo yao kwenye skuli mbali mbali wanazotoka.

Dr. Khalid aliwatoa hofu Wazazi wa Watoto hao kwamba Gari zilizoandaliwa zimepangwa kuwachukuwa  watoto hao na kuwapeleka kwenye Skuli zao waanze masomo kama kawaida na kuwarejesha Kambini  baada ya kumaliza masomo yao kwa kila kipindi watachokuwapo kambini hapo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s