Jeshi la Polisi lawamani

MRATIBU wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Hemed Khamis akizungumza na wapiganaji wa jeshi la Polisi wa mkoa wa kaskazini Pemba, wa mwanzo kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo, Mohamed Sheikhan, akifuatiwa na kamanda ‘RCO’ Kheir na afisa mipango wa ZLSC, Khalifan Amour
Mratibu wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Hemed Khamis akizungumza na wapiganaji wa jeshi la Polisi wa mkoa wa kaskazini Pemba, wa mwanzo kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo, Mohamed Sheikhan, akifuatiwa na kamanda ‘RCO’ Kheir na afisa mipango wa ZLSC, Khalifan Amour
Jumatano 6 APRIL 2015
Imeelezwa kwamba Jeshi la polisi nchini ndio linaloongoza katika ukiukwaji wa maadili katika majukumu yake na ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini.  

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kamisheni ya Mafunzo ya Jeshi la Polisi Zanzibar, SP Ali Abdalla Kitole huko Migombani katika ukumbi wa huduma za sheria kwenye mafunzo yaliyowashirikisha maofisa wa jeshi la Polisi na wasaidizi wa sheria ambayo yalijadili suala la haki za binaadamu.
Amesema utafiti uliofanywa mwaka 2013 umebainisha kuwa jeshi hilo linaongoza katika ukiukwaji wa maadili ya katika kazi zao lakini pia kwenye kuvunja haki za binadamu na raia.
Mkuu huyo alisema utafiti huo uliofanywa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar (ZLSC) na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC), ambapo jeshi hilo limeongoza kati ya taasisi kumi zilizofanyiwa utafiti huo.
Aliwaambia maafisa wa jeshi hilo na asasi nyengine za kiraia kwmaba kwa mujibu wa utafiti huo, jeshi hilo limebainika kuongoza katika vitendo vya rushwa kwa kushika nafasi ya kwanza likijikusanyia asilimia 52.4, ikifuatiwa na mahakama ambayo ilipata asilimia 38.2.
Aidha, SP Kitole alisema utafiti pia ulibainisha jeshi hilo limekuwa na kawaida ya kutumia nguvu kubwa hadi kuua ambapo kwa wakati huo ilibainika watu 31 waliuawa mikononi mwa maofisa wa polisi huku wengine 48 wakipata ulemavu wa maisha.
Polisi huwaadhibu hadi kuwapa ulemavu washukiwa wa uhalifu wanapokuwa kizuizini na pia kuna baadhi ya taarifa wanawake kubakwa wakiwa chini ya uangalizi wa Polisi”, SP Kitole aliwaeleza maaofisa hao katika mafunzo hayo.
SP Kitole ambaye alikuwa akiwasilisha mada iliyoelezea maadili ya jeshi la Polisi katika kusimamia haki za binaadamu, alisema jeshi hilo limebainika kuingilia uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano.
Salum Abdallah akizungumza na viongozi wa dini
Afisa Habari wa Kituo cha Huduma za Sheria, Salum Abdallah akizungumza na viongozi wa dini
Alifahamisha kuwa tatizo jengine lilibainika ni pamoja na baadhi ya maofisa wa jeshi hilo kuwa na tabia ya kuzisuluhisha kesi hasa zile zinazohusu udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Kutokana na hali hiyo jeshi la polisi limekuwa likitupiwa lawama mara kwa mara kutokana na kukiuka haki za binadamu kwa vile wanakwenda kinyume na maadili ya kazi zao”, alisema SP huyo.
Mkuu huyo alisema Kamisheni Mafunzo ya Jeshi hilo Zanzibar haifurahii kabisa kuona vitendo vya ukiukwaji wa maadili vinafanywa na watendaji wake, kwani vitendo hivyo kinyume na maadili na ni kinyume na haki za binadamu.
Alifahamisha kuwa sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 inaeleza kuwa ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na unaoheshimika, watumishi wa umma wanapaswa kuufuata kanuni za maadili hayo hivyo kwenda kinyume na maadili hayo ni kukiuka haki za binadamu.
Aidha alifahamisha kuwa kuendelea kuwepo kwa ukiukwaji wa maadili unapelekea kuondoa imani kwa wananchi kwa serikali yao pamoja na jeshi hilo.
Kuwepo kwa hali hiyo ndio inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kujichukulia sheria mikononi na kupelekea umwagikaji wa damu”,alisema.
Kwa upande wa mkufunzi kutoka chuo cha Polisi Zanzibar, Mohammed Kombo alisema ukiukwaji wa haki za binadamu ni ule unaofanyiwa vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na matakwa ya sheria na kusababisha kukosa haki za msingi.
Alisema sheria na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa imepitishwa au kutungwa katika ngazi zote ili kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu zinafuatwa na sio vinginevyo.
Hata hivyo, alifahamisha kuwa askari polisi wamepewa mamlaka kisheria kukamata na kuweka kizuizini mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria hivyo, kukiuka kufuata sheria ndio kunakopelekea uvunjifu wa haki za binadamu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s