Chifu Wanzagi: CCM isiibeze Ukawa

Chifu wa Wazanaki, Joseph Wanzagi (kulia) akizungumza na waandishi na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, Tabata Relini, jijini Dar es Salaam jana. Na Mpigapicha Wetu
Chifu wa Wazanaki, Joseph Wanzagi (kulia) akizungumza na waandishi na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, Tabata Relini, jijini Dar es Salaam jana. Na Mpigapicha Wetu

Dar es Salaam. Chifu wa Wazanaki, Joseph Wanzagi amasema CCM haitakiwi kuvibeza vyama vya upinzani hasa baada ya kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), huku akisema atakuwa mtu wa kwanza kumshauri Makongoro Nyerere kugombea urais wakati ukifika.

Chifu Wanzagi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi kwenye ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen.

Kiongozi huyo wa kimila alisema hivi sasa Ukawa ina nguvu kubwa tofauti na wakati vyama hivyo vilipokuwa havijaungana na kutaka pande zote mbili kuheshimiana licha ya tofauti zao za kiitikadi.

“Hata mimi naamini kuwa mgombea atakayeteuliwa na CCM ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuwa Rais, lakini Chama cha Mapinduzi kisibeze wapinzani, hasa baada ya kuungana na kuanzisha Ukawa,” alisema Chifu Wanzagi alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa chama hicho tawala kinapoteua mgombea ni kama kimemtangaza Rais wa Tanzania.

Vyama vinavyounda Ukawa- Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD- vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia kwenye nafasi ya urais hadi udiwani na tayari umoja wao ulifanya kazi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambako vyama hivyo vilitwaa viti kwenye maeneo mengi ambayo CCM ilikuwa inayashikilia.

Kiongozi huyo ambaye anatoka kwenye ukoo wa Nyerere alisema si mkereketwa sana wa masuala ya kisiasa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa ushindani wa kisiasa lakini anaamini CCM itashinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Alisema anakubaliana na msimamo wa Mwalimu Nyerere kwamba CCM ikisimamisha mgombea wa urais, ndiye anakuwa rais na anaamini mgombea atakayepitishwa na chama hicho kikongwe atashinda.

Makongoro kugombea

Kuhusu Makongoro, aliyemtaja kuwa ndiye mhimili wa familia ya Nyerere kisiasa, Chifu Wanzagi alisema: “Kwenye familia ya Nyerere, hakuna mwanasiasa mzuri zaidi ya Makongoro na kama hatoshi kwa nafasi hiyo, basi familia ya Mwalimu haina mwanasiasa tena.

Tunasikia anatajwa kwenye vyombo vya habari na inawezekana ana nia ya kugombea urais, ila sisi hajatuambia. Lakini wakati ukifika, hata kama familia haitamshawishi, mimi nitakuwa wa kwanza kumwita na kumshauri achukue fomu ya kugombea urais,” alisema Chifu Wanzagi.

Makongoro anatajwa kuwa mmoja wa watu wanoshawishiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais kwa ajili ya kuunganisha makundi yaliyoibuka ndani ya CCM kutokana na harakati za kuwania nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini. Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa hajatangaza nia wala kuonyesha harakati zozote za kutaka kumrithi Rais wa sasa, Jakaya Kikwete ingawa amekuwa akielezewa kuwa ni mtu ambaye anaandaliwa kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Chifu huyo, ambaye pia ni kiongozi wa dini, alisema msukumo huo unatokana na sifa alizonazo Makongoro.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s