Maafa ya Mvua: Wawili wafariki na wengi wakosa makaazi

Mama huyu ni mmoja tu kati ya waliopata wananchi  wengi wa Zanzibar waliopata maafa ya mvua iliyoanza jana asubuhi na kuendelea hadi leo
Mama huyu ni mmoja tu kati ya waliopata wananchi wengi wa Zanzibar waliopata maafa ya mvua iliyoanza jana asubuhi na kuendelea hadi leo

WATU wawili wamefariki dunia na wawili kuumia vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta juzi baada ya mvua kubwa kunyesha kwa muda wa saa 3 mfululizo katika visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud amesema mvua iliyonyesha imeleta maafa makubwa ambapo baadhi ya maeneo wakaazi wake wamekosa makaazi baada ya mvua hiyo kuathiri.

IMG-20150504-WA0044

Akiwataja waliopoteza maisha ni Juma Hamad (25) mkaazi wa Kinuni na mtoto mwenye umri wa miaka minane ambapo maiti yake tayari imeshazikwa wakati maiti ya Hamad haijapatikana na juhudi za kutafuta mwili wake zinaendeleo.

Aboud alisema maeneo ambayo yameathirika ni 17 ikiwemo Magomeni, Jangombe, Nyerere, Sebleni Sogea, Mwanakwerekwe, Welezo, Kisauni, Tomondo, Mombasa, Kinuni, Mtopepo, Chumbani, Kwahani, Mpendae, Bububu na Kwahani.

IMG-20150503-WA0078

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia sehemu mbali mbali nyumba zilizoanguka, kuta nyingi kuwa chini, miti kukatika matawi na mengine kungoka na baadhi ya barabara kujaa maji na kukosa njia za kupita katika maeneo ya Mjini huku baadhi ya mitaa wakaazi wake wakiwa wamehama nyumba zao na kuomba msaada kwa ndugu jamaa na marafiki zao.

Aboud alisema kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Zanzibar, kiwango cha mvua kilichonesha kwa muda wa saa tatu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana na wastani wa milimita 172.2 kiwango ambacho ni kikubwa sana kutokea.IMG-20150503-WA0081

“Hali hii imesababisha mafuriko katika maeneo mbali mbali hasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea athari kubwa katika maeneo hayo ikiwemo vifo, uharibifu wa nyumba na makaazi na upotevu wa mali na mifugo” alisema Aboud.

Hata hivyo alisema mvua bado zinaendele kunyesha na hakuna uhakika zinamalizika lini lakini aliwataka wananchi kuchukua tahadhari za kujiepusha na athari hizo.

Aliwashauri wazazi kuwaangalia watoto wao wasicheze katika maeneo yanayotuama maji na kwa wale wananchi wenye kuishi katika maeneo ya bondeni ni kuyahama maeneo hayo katika kipindi hiki ambacho mvua hizo zinaendelea.

Aidha wananchi wenye kuchimba mashimo katika maeneo ya makaazi wanapaswa kuwa waangalifu kwa kuyafunika mashimo hayo kwa haraka ili yasilete madhara kwa wananchi wengine katika kipindi hiki.

Aboud alisema serikali inawashauri wananchi kuchemsha maji wanayotumia na kuhifadhi vyakula ili kuepusha maradhi mbali mbali ya mripuko sambamba na kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za afya ikiwemo usafi binafasi na wa maeneo yanayowazunguka wakati huu wa mvua zinazoendelea.

Akizungumzia suala kiasi gani cha athari zilizotokea Aboud alisema hadi sasa hakuna tathimini lakini serikali imepitia maeneo yote yalioathirika na inaendelea kufanya tathmini ya kina ili kujua hasara ambayo wananchi wameipata kutokana na matukio hayo.

Aidha alisema serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha kuwa hali ya maisha ya wananchi inarudi kama kawaida.

IMG-20150504-WA0035

“ Kwa niaba ya Serikali nachukua fursa hii kuwapa mkono wa pole wale wote waliopoteza jamaa zao kutokana na maafa haya Mwenyeenzi Mungu awape moyo wa subira katika wakati huu mgumu wa msiba na tunamuomba Mwenyeenzi Mungu azilaze roho za marehemu pahala pema na walojeruhiwa wapote haraka” alisema Aboud.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s