Salma Said apewa tunzo

Human Rights Defender imetoa tunzo kwa watu watatu akiwemo Mmiliki wa Mtandao huu Bi Salma Hamoud Said ni miongoni mwa watu watatu waliopewa tunzo ya mwanamke jasiri katika utetezi wa haki za binaadam, mwengine ni David Kafulila na Maanda Ngoitiko  jana katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plaza
Human Rights Defender imetoa tunzo kwa watu watatu akiwemo Mmiliki wa Mtandao huu Bi Salma Hamoud Said ni miongoni mwa watu watatu waliopewa tunzo ya mwanamke jasiri katika utetezi wa haki za binaadam, mwengine ni David Kafulila na Maanda Ngoitiko jana katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plaza

Human Rights Defender imetoa tunzo kwa watu watatu akiwemo Mmiliki wa Mtandao huu (zanzibaryetu) Bi Salma Hamoud Said ni miongoni mwa watu watatu waliopewa tunzo ya mwanamke jasiri katika utetezi wa haki za binaadam, mwengine ni David Kafulila na Maanda Ngoitiko jana katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plaza

Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow limemng’arisha Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi),  David Kafulila baada ya kutunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kufichua ufisadi huo uliohusisha uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Katika sakata hilo, mawaziri wawili walipoteza nyadhifa zao pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuwahusisha na sakata hilo. Maofisa wengine kadhaa wa Serikali wamesimashwa au kufunguliwa mashtaka kutokana na kuhusika kwao kwenye ufisadi huo.

Salma Said, David Kafulila na Maanda Ngoitiko waliopewa tunzo wa kutambuliwa mchango wao katika kutetea haki za binaadam.
Salma Said, Maanda Ngoitiko na David Kafulila waliopewa tunzo ya kutambuliwa mchango wao katika kutetea haki za binaadam.

Sakata hilo lililoteka kwa kiasi kikubwa mkutano wa Bunge wa 16 na 17 kabla ya kufika bungeni,  liliibuliwa na Gazeti la The Citizen, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd na Kafulila kuwasilisha hoja ndani ya Bunge ili kujadiliwa.

Tuzo aliyopewa Kafulila jana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu (THIRD-Coalition), ni moja kati ya tuzo tatu zilizotolewa kwa Watanzania walioonyesha ujasiri katika kutetea haki za binadamu nchini.

Wengine ni Maanda Ngoifiko wa asasi ya kiraia, inayotetea haki za binadamu ya PWC kutoka  Loliondo  wilayani Ngorongoro, na Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Salma Said aliyetishiwa kuuawa baada ya kuonyesha msimamo wa kukataa shinikizo la kukubaliana na muundo wa Muungano wa serikali mbili wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.cheti

Kwa mujibu wa THIRD-Coalition, vigezo vilivyotumika kuwapata washindi hao vilizingatia mazingira ya kazi na hali hatarishi aliyokutana nayo mshindi wa tuzo hiyo, ikiwamo taarifa zilizokusanywa kupitia ripoti za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mwaka jana.

Baada ya kukabidhiwa, Kafulila alisema tuzo hiyo ni mwanzo wa hatua nyingine ya kuendelea kuibua ufisadi ndani ya Serikali.

“Nimepata ujasiri na kuamini kwamba siko peke yangu katika vita hii, nashukuru kupata tuzo hii, lakini nashukuru zaidi ushirikiano nilioupata kwa mhariri wa gazeti la The Citizen, ambaye alinipatia nyaraka nne za kuanzia,” alisema Kafulila.

Ngao hii ni ishara ya kujikinga dhidi ya maadui wanaokuja na ubaya wao
Ngao hii ni ishara ya kujikinga dhidi ya maadui wanaokuja na ubaya wao dhidi yangu

“Hata hivyo, ninasikitishwa kuona bado Tanesco wakiendelea kulipia Dola 4 bilioni za capacity charge kwa kampuni hiyo ya ITPL, wakati hukumu iliyotolewa na Mahakama ya ICSID ya Uingereza Februari 12, mwaka jana inasema haikuwa sahihi tozo hiyo, lakini bado kiwango hicho kinaendelea kulipiwa.”

Salma Said akitoa neno la shukurani na kuelezea msimamo wake juu ya utetezi wa haki za binaadam kwamba tunzo hiyo imezidi kuwapa ari na nguvu zaidi za kufikia mafanikio
Salma Said akitoa neno la shukurani na kuelezea msimamo wake mbele ya mabalozi juu ya utetezi wa haki za binaadam kwamba tunzo hiyo imezidi kuwapa ari zaidi za kufikia malengo na katu hawatarudi nyuma katika kupigania haki za wanyonge. “I will never give up”

Salma alisema pamoja na vitisho ambavyo bado ameendelea kukutana navyo mpaka sasa kutoka kwa baadhi ya wabunge wa lililokuwa Bunge la Katiba, bado msimamo wake utaendelea kuwa palepale.

Aidha, alisema vita iliyopo kwa sasa imehamia kwenye harakati za Baraza la Katiba la Zanzibar ambalo linaendesha elimu kwa Wazanzibari kuhusu Katiba Inayopendekezwa. “Mimi ni mjumbe wa Baraza hilo na kwa sasa hawapendi kuona tukielimisha ukweli wa Katiba hiyo na badala yake wanataka kueleza mazuri tu. Hilo tumesema haliwezekani.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s