CCM inatengeneza wapinzani wake yenyewe

Ipo siku utabiri huo utatimia, utatimia kwa namna gani, mimi sifahamu. Wapo waliojaribu kutoka CCM na kuanzisha vyama vyao au kujiunga na vyama vingine vya siasa vilivyopo, pengine mshindo wao haukuweza kuing’oa CCM, lakini ni makosa tukisema kuwa mshindo wao ulikuwa mdogo
Ipo siku utabiri huo utatimia, utatimia kwa namna gani, mimi sifahamu. Wapo waliojaribu kutoka CCM na kuanzisha vyama vyao au kujiunga na vyama vingine vya siasa vilivyopo, pengine mshindo wao haukuweza kuing’oa CCM, lakini ni makosa tukisema kuwa mshindo wao ulikuwa mdogo

Hawra Shamte

Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema: “Hakuna vyama vya upinzani vyenye uwezo wa kuing’oa CCM madarakani, upinzani wa kweli utatoka CCM, wenyewe kwa wenyewe watatofautiana kisha wataanzisha chama chao.”

Ipo siku utabiri huo utatimia, utatimia kwa namna gani, mimi sifahamu. Wapo waliojaribu kutoka CCM na kuanzisha vyama vyao au kujiunga na vyama vingine vya siasa vilivyopo, pengine mshindo wao haukuweza kuing’oa CCM, lakini ni makosa tukisema kuwa mshindo wao ulikuwa mdogo.

Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa mwanachama nguli wa CCM, alipoondoka huko alijiunga na CUF.

Kusema kweli CUF ilipata nguvu kisiasa Maalim Seif alipojiunga nayo. Mpaka leo CUF si chama cha kukidharau hata kidogo, kwani huko Zanzibar kinaiendesha CCM mchakamchaka.

Dk Willibroad Slaa naye alikuwa CCM, alipoondoka huko alijiunga Chadema. Nguvu za Dk Slaa Chadema si za kuzibeza hata kidogo, hivi sasa Chadema ni chama mbadala wa CCM kwa Tanzania Bara.

Vijana wengi wanajiunga na Chadema au wanakipenda chama hicho kwa sababu kwa sasa kinawapa matumaini, viongozi wake wanazungumza lugha yao. Wanaonekana kama kimbilio au mkombozi, ndiyo maana Chadema inaichachafya CCM katika maeneo mengi ya miji.

CCM nao wana kadhia zao za ndani. Unapokuwa na mawazo tofauti na wao, wanakuona kama si mwenzao, hivyo wanakufurusha.

Walifanya hivyo kwa Mansour Yusuf Himid na sasa wamefanya hivyo kwa Mzee Nassor Moyo.

Pengine hawajafanya makosa kwa sababu “ndege wenye mbawa zinazofanana huruka pamoja,” sasa wewe ukiwa mbawa zako zina rangi tofauti na zao, vipi utaruka pamoja nao?

Bila shaka watakufurusha tu, kwa sababu si mwenzao, nao wana namna zao za kujilinda wasiingiliwe na maadui, hivyo wanamtilia shaka kila mwenye rangi tofauti na yao.

Hiyo ndiyo silika ya kimaumbile, na hata vyama vya siasa navyo vina silika kama hiyo, ukiwa mwanachama lazima ujenge uaminifu kwa chama na ujenge kukubalika, ukikosa sifa hizo, lazima wakushughulikie, au ukiwa kigeugeu usiyetambulika kama ni ndege au mnyama pia watakutilia shaka na hatimaye kukuengua, ili wao waendelee kubaki salama.

Lakini kwa misimamo waliyoionyesha Mansour na Moyo, yao haikuwa misimamo ya upinzani bali ilikuwa misimamo ya uzalendo kwa nchi yao.

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “CCM inatengeneza wapinzani wake yenyewe”

 1. Ukweli ni kwamba Waliojitowa CCM walijin`gatuwa kwa sababu zao ;moja wapo ikiwa
  ni mivutano ya Itikati na Kinyan`ganyoro cha kupata vyeo vya juu ,uchu wa madaraka
  na wengine kuwa na hamu ya Urais ikiwa ni Visiwani au Bara.

  Pili ,CUF kina nguvu sana Visiwani na hiyo ni kutokana na sababu maalum za “Itikadi
  Sugu Za hisiya za Kiuvisiwani” ambazo ni mabakia ya vyama na wafuasi wa vyama vya
  siasa vya kale “. Chama cha CUF-hakina nguvu zozote Tanzania Bara.
  Ushahidi tosha ni matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana wa serikali za mitaa .

  Chama cha Chadema kina nguvu sana Bara na kimejengwa kwa shawishi nyamala za
  Ujitwikaji mada za kuunda umaarufu hasa kwenye miji mikuu ambako zipo shida nyingi
  makaazi,ukosefu wa ajira ,huduma na mchan`ganyiko wa mivutano ya Ukabila.

  Matamko makali-makali ya kisiasa ya Uchadema mara nyingi huwa kidan`ganyifu yanawapa tamaa wakosa ajira ,na wenye njaa huwa wanazikubali ahadi hizo za kisiasa ambazo kamwe
  haziwezi kukamilishwa – kama zile za eti kutatuwa matatizo yote mnamo siku 100 zinzo
  tolewa na CUF -Visiwani .

  Kuhusu Kufukuzana Uwanachama ,hili ni jambo la kawaida kwa vyama vyote nchini.CUF
  chadema,Mageuzi na haiwezi kuwa ni ajabu kwamba CCM nao wanafukuzana.Na kwa nini
  iwe ni ajabu hata ikiwa Nyerere aliyasema ?.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s