Tunahitaji mabadiliko ya mfumo haraka iwezekanavyo

Wananachi mbali mbali waliokuwa wakionesha mikono juu kuashirikia kutaka mabadiliko katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na UKAWA Mjini Unguja
Wananachi mbali mbali waliokuwa wakionesha mikono juu kuashirikia kutaka mabadiliko katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na UKAWA Mjini Unguja

Hawra Shamte

Siasa nchini sasa zimefikia wakati wake, wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu. Zitto Kabwe amejiunga na chama kipya, kichanga cha ACT- Wazalendo. Ni chama kilichopata usajili wake hivi karibuni pia kuchagua viongozi wake wakiwa na mrengo wa ujamaa wa kimaendeleo.

Zitto anasema kuwa pamoja na udogo wao, wasidogoshwe (don’t under-estimate us) kwani wanaweza kufanya makubwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa siasa za nchi hii.

Zitto anasema katika mwaka huu wana matarajio ya kupata majimbo angalau 20, hiyo siyo idadi ndogo hata kidogo kwa chama kichanga.

Kama mzaha, Zitto kavuta watu katika mkutano wake wa Iringa watu walikuwa nyomi, huko Kigoma ambako dhamira yake ni kuyachukua majimbo yote nane, vyama vingine visipokuwa makini vinaweza kuachwa midomo wazi!

Mwaka huu vyama vya siasa vitakuwa katika mirengo miwili ya upinzani. Kwanza vyama vya upinzani na dhamira yao ya kuing’oa CCM. Pili viko vyama vya upinzani vilivyo nje ya Ukawa ambavyo vitashindana na CCM na Ukawa kwa wakati mmoja.

Hivyo, ndiyo kusema kuwa hivi sasa siasa hazielekezwi tena kwa CCM pekee, bali viko pia vyama vinavyotafuta fursa ya kujiainisha kuwa ni tofauti na vyama vingine vya upinzani kisera na kimwelekeo ingawa vyote vina lengo moja la kuing’oa CCM madarakani.

Zitto anasema kuwa umefika wakati wa kubadilisha mfumo wa uendeshaji nchi kwa sababu kinachofanya nchi hii isiendelee ni mfumo ulioganda, hivyo dawa yake ni kuufumua wote na kuunda mpya.

Mfumo wetu wa kuendesha nchi hauna ufuatiliaji, kama mtu anaweza kuchota Sh300 bilioni kutoka Benki Kuu, ambazo kimsingi si zake, akazitawanya atakavyo na wala serikali isishituke, hakika nchi hiyo mifumo yake ya kifedha ni mibovu, haina udhibiti.

Kwa mujibu wa ripoti ya Ernest & Young Company waliofanya kazi kwa niaba ya ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2008, zaidi ya Sh90 bilioni zilichotwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payment Arrears-EPA) na kampuni 13 zilizotumia hati, kumbukumbu na nyaraka feki kukamilisha wizi huo.

Bahati mbaya ni wachache ndiyo waliobambwa na mkono wa sheria, wengine waliambiwa warudishe fedha walizochota kwa hiari yao. Jamani, huo ni mfumo gani wa uwajibikaji wa kisheria?

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s