Butiku: Yaliyonyofolewa Katiba Mpya yarudishwe

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusogeza mbele tarehe ya Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa, iwe mwanzo wa kutafakari na ikiwezekana kurejesha mambo ya msingi yaliyoondolewa katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alitangaza kusogezwa mbele kwa tarehe hiyo, hadi itakapotangazwa tena. Awali, ilipangwa kuwa Aprili 30.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Butiku aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba, alisema kuahirishwa kwa upigaji Kura ya Maoni ni nafasi pekee kwa NEC kujipanga upya na kuhakikisha wananchi wanaandikishwa kwa kiwango kikubwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema pia ni wakati mwafaka kuwapo kwa majadiliano ya kina ili kuangalia nini kinatakiwa kirudishwe kutoka katika vile vilivyoenguliwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba kama itawezekana.

Wakati Butiku akisema hayo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema kipindi hiki cha kusitishwa Kura ya Maoni, kitumike kuingiza mambo makuu manne yaliyonyofolewa kwenye Katiba Inayopendekezwa.

Jana gazeti hili liliripoti kuwa kuahirishwa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa kumewafungulia viongozi wa Ukawa kuishinikiza Serikali kuiboresha Katiba ya mwaka 1977 katika maeneo manne ili kuondoa mvutano katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Mambo manne yanayodaiwa na Ukawa ni; ushindi wa urais kuamuliwa kwa asilimia zaidi ya 50, kuwapo kwa mgombea binafsi katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, tume huru ya uchaguzi na matokeo ya urais kupingwa mahakamani. Umoja huo unasema mambo hayo ni sehemu ya maafikiano baina yake na Rais Jakaya Kikwete Septemba 8, mwaka jana.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema maboresho yaliyofanyika chini ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ni ya lazima ili kufanikisha uchaguzi huo kabla ya kupitishwa kwa Katiba Mpya na kuondoa uwezekano wa vurugu.

Katika kikao hicho, Mbatia alisema walitiliana saini kuwa iwapo uchaguzi wa mwaka huu utafanyika kwa kutumia Katiba ya 1977, Bunge lingekutana Novemba mwaka jana kufanya marekebisho hayo ya 15 ya Katiba na endapo hilo lingeshindikana, basi lingekutana Februari, jambo ambalo pia halikufanyika.

Kauli ya Butiku

“Rasimu ya pili ya Katiba iliyotolewa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo mimi nilikuwa mjumbe, ilikuwa imebeba mambo mengi na muhimu ya wananchi ambayo yaliondolewa, hivyo huu ni wakati mwafaka kutafakari kwa kina jinsi ya kuyarudisha,” alisema Butiku.

Alisema hiyo pia ni nafasi kwa wananchi ambao baadhi yao walikuwa wanaburuzwa, ama na chama au na mtu fulani kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa ambayo hawajaisoma na kuielewa kufanya hivyo.

 Chanzo: Mwananchi
Advertisements

2 Replies to “Butiku: Yaliyonyofolewa Katiba Mpya yarudishwe”

  1. Reblogged this on Haki Sawa kwa Wote and commented:
    Msimamo wa CUF kama ulivyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni kwamba kwa makusudi kabisa CCM iliuteka nyara mchakato mzima wa Katiba Mpya na hivyo kulinyima uhalali wa kitaifa zoezi zima. “Katiba ni tendo la maridhiano”, anasema Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, na hivyo bila maridhiano ya kitaifa, hakuwezi kuwa na katiba.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s