Vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume

Dk Shita Samwel
                                                       Dk Shita Samwel

Tunaendelea na sehemu ya pili ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume. vyakula vya nafaka ambavyo vimesheheni nishati nyingi, nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.

Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu pia huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kuongeza nguvu zake za kiume.

Kula nafaka zisizokobolewa kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri kiafya zina saidia kutokupa mwili wa mafuta mengi, ikumbukwe uwapo wa mafuta mabaya yanaharibu mishipa ya damu ikiwamo ya uume.

Tangawizi ni aina ya kiungo mizizi ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Mzunguko unapokuwa mzuri huwezesha damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi ikiwamo uume.

Tangawizi imekuwa ikitumika sana maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.

Viungo ambavyo viko katika pilau ni mojawapo ya vitu ambavyo miaka na miaka imetumika maeneo ya Asia na Amerika ya Kaskazini kama viungo vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume.

Vyakula vinginevyo

Pemigranate ni aina ya matunda yenye rangi nyekundu na mwonekano kama apple.

Tunda hili husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumwongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

Hivyo humfanya mtumiaji kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi. Mvinyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu huku ikimwondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa.

Hii ndiyo sababu kubwa kuikuta ikiweka vyumbani katika hoteli nyingi kubwa duniani. Nchi kama Italia mvinyo ni kinywaji ambacho hakikosekani mezani yote kutokana na kuaminika miaka kwa miaka.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s