Utovu wa adabu uliokithiri

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ametangaza kuwa huduma za uzazi kwa akina mama wajawazito wanaokwenda kujifungua katika hospitali za umma Unguja na Pemba zitafanyika bure.Dk. Shein aliyasema hayo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tunguu, wakati alipokuwa akitowa majumuisho ya ziara yake ya siku tatu aliyoifanya katika Mkoa wa Kusini Unguja na kusisitiza kuwa huduma hizo hazitolipiwa tena.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika moja ya ziara zake akisisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi lakini licha ya kauli hizo za mara kwa mara kwamba watendaji wa serikali wasifanye kazi kwa mazowea badowatumishi wa umma hawawajibiki wala kuwajibishwa 

Utovu wa adabu uliokithiri kwa watoa huduma wa Mamlaka mbalimbali Zanzibar
Kuna kadhia kubwa visiwani Zanzibar, hasa katika sekta ya utoaji huduma. Hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku kwa vile wananchi walio wengi hawapati tahfifu wala ufumbuzi wa kero wanazokumbana nazo wanapotaka huduma za aina mbalimbali iwe katika vyombo vya umma au taasisi binafsi. Hususan wafanyakazi wa taasisi za umma pamoja wamekuwa watovu wa adabu na hawaonyeshi nidhamu katika utoaji wa huduma.

Suala la huduma kuwa haki ya msaka huduma halipo na wala halizingatiwi. Wafanyakazi au wahudumu wengi hawana mkabala wala  lugha inayostahili kwa mtoa huduma.Wengi ni jeuri wababe na wanajibu na kuthubutu kusema kinachowajia bila ya kujali wanazungumza na nani na wakati gani. Kwa bahati mbaya hakuna mamlaka wala uongozi unaodhibiti utovu wa adabu huo. Vyombo vinavyosimamia huduma mahsusi kama vipo vimekuwa butu na hata vikiombwa havina msaada. Kilichopo ni watoa huduma kusuta wasaka huduma na kujinadi kuwa hawamuogopi mtu au mamlaka yoyote hivyo mlalamikaji aende anapokwenda hapatakuwa kitu!

Mnamo tarehe 7 Fenruaru nimekabili na utovu wa nidhamu wa hali ya juu nilipokuwa narejea nchini kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa vya Zanzibar huko Kiembe Samaki. Niliwasili na ndege ya Precision kutokea Nairobi na tulipokuwa tunapita kukaguliwa na mafaisa wa Uhamiaji mmoja wa maofisa hao ambaye alikuwa hayupo nyuma ya dawati la wakaguzi alitupita huku akiuuliza kwa sauti “Ushamtia madole huyu?” Kwa vile ndege ilijaa wageni mimi nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuhudumiwa. Alinipita karibu kabisa akitamka maneno hayo huku yakifuatiwa na kicheko.

Hakika matamshi kama hayo si sehemu yake na hayajastahili. Kweli, kijana huyu, afisa wa Uhamiaji alidhani kakiweza sana Kiswahili na hatutamuelewa kusudio lake? Kweli alidhani kila mgeni hafahamu Kiswahili au hatuelewi anamaanisha nini? Kibaya zaidi sijamsikia hata mtu mmoja kati ya wenzake (au msimamizi wao) kumtanabahisha dhidi ya kauli yake ambayo si tu ilikera lakini pia ni ya kudhalilisha kwani akiyatumia kwa sisi wanawake tuliokuwa tukikaguliwa.

Kwamba mtoa huduma ya jamii kathubutu kufanya jambo ambalo kawaida watoto ndio hulifanya wakiwa mtaani kwao wanacheza linaonyesha namna hatuzipi kazi tunazozisimamia heshima. Pia inaonyesha kuwa hutuwaheshimu wateja wetu. Mpaka lini tutaendelea kuwalea watu wasiojua kuenzi nafasi walizopewa kama amana ya utumishi? Hivyo, kweli hakuna wasimamizi wa kuwasimamia na kuwathibiti wafanyakazi wao?
Imeandikwa na Mkereketwa wa Zanzibar

 

One Reply to “Utovu wa adabu uliokithiri”

  1. Assalaamu alaykum.
    Ndugu yangu Mkereketwa wa Zanzibar pole kwa maswahibu hayo. Maudhui ya uwasilishaji wako huu ni wa haki na wa mantiki sana, mimi ni shuhuda wa mengi yanayotokea hasa hapo ulipo pataja Kiwanja cha ndege cha Zanzibar na kweli juhudi kubwa zinahitajika kubadili mitazamo ya jamii yetu.

    Ila nadhani uwasilishaji wako umetumia lugha yabisi kidogo kama kwamba pale ulipokerwa sana nawe sasa unajibu lile pande la tusi ulilokwaana nalo. Sikukosowi ila nakukumbusha tu yatakapo kukuta kama hayo ni bora kubakia kwa muda kidoogo ukapoa kuliko kukimbilia kalamu.

    Isibu sadaka yangu.

    Naitwa Khatib.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s