Tamasha la Uzalendo Zanzibar

Balozi Seif akitoa hotuba ya kulizindua Tamasha la Uzalendo Tanzania kwenye uwanja wa Amani lililoshuhudia na mamia ya wapenda burdani hapa Zanzibar.
Balozi Seif akitoa hotuba ya kulizindua Tamasha la Uzalendo Tanzania kwenye uwanja wa Amani lililoshuhudia na mamia ya wapenda burdani hapa Zanzibar.

Kundi la  wasanii kumi na moja wa kizazi kipya  Ndani ya Tanzania leo limeuvamia uwanja wa michezo Amani kufanya Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015.

Tamasha hilo lililoasisiwa Mwaka Jana  Mjini Dodoma na Rais wa Jamuhuri ya Muungano w Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lina lengo la kueneza ujumbe wa kudumisha amani na Umoja Miongoni mwa Watanzania wote.

Mamia ya Vijana na wapenda burdani walionekana kumiminika katika uwanja huo wa amani kushuhudia waimbaji maarufu wa Kikazi kipya wakifanya vitu vyao jambo ambalo liliwafanya wengi wa mashuhuda hao kuwacha viti vyao na kuanza kuserebuka.

Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba wasanii Nchini Tanzania wana dhamana kubwa katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kupitia fani yao ya sanaa.

Akilizindua Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema wasanii ndio kioo cha jamii kinachoweza kutumika katika kufikisha ujumbe na hata masuala ya maendeleo ya Kijamii.

Alisema mchango wa wasanii katika jukumu kubwa linalolikabili taifa ndani ya mwaka huu wa 2015 kwenye kura ya maoni sambamba na uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba ni muhimui sana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wasanii hao kuhakikisha kwamba suala la Amani  linakuwa ndio dira itakayowapa mwanga wa kuendeleza shughuli zao za sanaa popote pale Nchini Tanzania.

Alisema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni kisiwa cha amani Duniani. Hivyo juhudi za pamoja kati ya wasanii na wananchi zinahitajika ili kuona lulu hiyo ya amani Nchini Tanzania inaendelea kudumu.

Mapema Mjumbe wa Kamati ya Tamasha hilo Nd. Shaib Ibrahim Mohammed alisema kwamba hilo ni tamasha la kwanza kufanyika hapa Zanzibar likiwa na ujumbe wa kuendelea kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani, Umoja na Upendo miongoni mwa Jamii hapa Tanzania.

Akitoa shukrani mwa niaba ya Kundi hilo Msanii Miki wa Pili alizishukuru na kuzipongeza Serikali zote mbili Nchini Tanzania kwa kufahamu umuhimu na mchango wa Wasanii.

Miki alisema fani ya sanaa ndani ya ardhi ya Tanzania ilikuwa ikitambuliwa kama kazi ya kihuni katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Alisema Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wana haki ya kupongezwa kwa kujenga historia ya kudumu iliyoainisha umuhimu wa kutambiliwa kwa kazi za wasanii na kupelekea kuingizwa ndani ya Katiba inayopendekezwa.

Chanzo: Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s