Rais Kikwete: Uvamia wa polisi una dalili za ugaidi

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya mapema kulipokucha wakiwasili eneo la tukio Westland Mall jijini Nairobi. ©AP
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya mapema kulipokucha wakiwasili eneo la tukio Westland Mall jijini Nairobi kwa kupambana na wanaoitwa Magaidi, nchini kwetu Tanzania wimbo wa ugaidi umeanza kuimbwa kidogo kidogo na serikali zetu za Tanzania na Zanzibar lakini wanasahau kwamba mtoto haimbiwi wimbo mbaya.

Dar es Salaam. Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amedokeza kuwa matukio ya watu wasiojulikana kuvamia vituo vya polisi, kupora silaha na kuwashambulia askari kuwa, “yana sifa za ujambazi na mwelekeo wa kigaidi.”

Akizungumza katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi jana, Rais Kikwete alisema hali ya usalama nchini ni nzuri kutokana na matukio hayo pamoja na mengine ya mauaji ya albino.

“Matukio haya yana sura mbili. Yana sura ya ujambazi, lakini pia baadhi yake yana dalili za ugaidi. Vyombo vyetu vya usalama vinaendelea kufanya kazi yake ya uchambuzi wa kila tukio na kulipa nafasi yake stahiki,” alisema Rais Kikwete.

Matukio yenyewe

Katika hotuba hiyo ya maneno 3,362, Rais Kikwete alitoa orodha ya matukio ya kuvamiwa vituo vya polisi kuwa katika kipindi cha miezi 12 jumla ya bunduki 38 ziliporwa na askari polisi saba kuuawa.

Alivitaja vituo vya polisi vilivyovamiwa kuwa ni Newala mkoani Mtwara ambako bunduki tatu ziliporwa, Ikwiriri katika Wilaya ya Rufiji (bunduki saba), Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga (bunduki tano), mbili zikiwa za polisi na tatu za raia zilizokuwa zimezihifadhiwa hapo.

Alisema katika Kituo cha Ushirombo Wilaya ya Bukombe bunduki 18 ziliporwa, ingawa baadaye zilipatikana zote.

Kadhalika, alisema katika maeneo ya Pugu Machinjioni na Tanga, askari waliokuwa katika shughuli za ulinzi na doria walishambuliwa na kuporwa silaha tatu.

Askari waliouawa

Katika matukio hayo, Rais Kikwete alitaja idadi ya askari saba waliopoteza maisha mmoja akitoka katika kituo cha Newala, Kimanzichana mmoja, Ikwiriri wawili na Ushirombo watatu.

Hata hivyo, Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kutoa pongezi kwa polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) kwa kazi nzuri ya kupambana na uhalifu nchini.

“Silaha zote 18 zilizoporwa Ushirombo zimepatikana na watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo wamekamatwa. Katika tukio la Tanga silaha moja kati ya mbili zilizoporwa imepatikana,”alisema Rais Kikwete.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s