Vijana Zanzibar kunufaika na ajira Qatar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mara baada ya kuwasili kutoka ziara yake ya Qatar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mara baada ya kuwasili kutoka ziara yake ya Qatar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema vijana wa Zanzibar sasa watanufaika na ajira mbali mbali nchini Qatar kufuatia ziara yake na baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaili uwanja wa ndege Zanzibar akitokea nchini Qatar, Maalim Seif alisema Qatar itatoa fedha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya kazi mbali mbali vijana wa Kizanzibari ambao baadaye wataelekea Qatar kufanya kazi hizo.

Makamu wa Kwanza wa Rais alisema tayari Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitia saini makubaliano na Qatar siku za nyuma, ambapo Watanzania watakwenda kufanya kazi nchini humo, na kwamba Wazanzibari ni miongoni mwa watakaonufaika na fursa hizo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa  Zanzibar Maalim  Seif Sharif Hamad akivishwa shada la maua  alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume  akitokea  nchini Qatar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akivishwa shada la maua alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea nchini Qatar

“Wametuahidi watatupatia fedha kwa ajili ya kuwaandaa vijana wa Wazanzibar kitaaluma ili hapo baadaye waende wakafanye kazi huko Qatar”, alisema Maalim Seif

Maalim Seif alisema imefika wakati Watanzania wawe na tabia ya kuchangaamkia fursa za ajira na kiuchumi zinazopatikana katika mataifa ya kigeni ili kupunguza uhaba wa ajira kwa wananchi, kama ambavyo yanafanya mataifa mengine mbali mbali, ikiwemo Kenya.

“Wakenya wamechangaamka sana ukiangalia kule sisi tuko wachache sana, tena wachache hao ni wale waliokwenda katika nchi hizo kwa kutumia njia zao wenyewe”, alisema Maalim Seif ambaye alikuwa ameambatana na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea nchini Qatar, wa kwanza (kushoto) Waziri wa Nchi katika Ofisi yake  Fatma Abdulhabib Ferej

Mbali na ajira, Makamu wa Kwanza wa Rais alisema Qatar itatuma timu ya wataalamu watakaokuja Zanzibar kwa ajili ya kuangalia maeneo yote ambayo Zanzibar iliomba isaidiwe ikiwemo ya kiuchumi na kijamii, ili kuona ni kwa namna gani wataweza kusaidia kufanikisha makubaliano hayo.

Alisema katika ziara hiyo Zanzibar iliomba kusaidiwa kukamilisha barabara ambazo hazijakamilika katika kiwango cha lami, kupatiwa utaalamu wa nishati ya umeme, upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa wa Mjini Magharibi, ujenzi wa uwanja wa ndege kisiwani Pemba pamoja na msaada wa kuimarisha Madrasa.

Maeneo mengine alisema wawekezaji wa nchi hiyo walifunguliwa milango kutumia fursa iliyopo kuwekeza vitegauchumi, ikiwemo katika sekta za utalii, viwanda vidogo vidogo na uvuvi wa bahari kuu.

Mwandishi wa habari wa Radio Adhana FM Said  Mussa Makame akimuuliza swali Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar

Maalim Seif amesema Zanzibar itaweza kupata mafanikio makubwa kufuatia ziara hiyo, iwapo haitazembea katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa, ambapo alisema Qatar imeonesha moyo wa dhati kuisaidia Zanzibar, ambayo watu wake wanafanana sana kiutamaduni.

Alieleza kuwa ziara hiyo imeonesha mafanikio makubwa kwa sababu Qatar imedhihirisha kuwa ina hamu kubwa ya kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na Zanzibar.

Alisema mazingira ya Zanzibar na Qatar yanafanana kwa sababu kwa miaka mingi kabla ya kugundua maliasili ya gesi asilia, ilikuwa ikitegemea uvuvi na kufuga chaza kwa ajili ya kupata lulu katika kuimarisha uchumi wake, lakini hivi sasa ni kati ya nchi tajiri zaidi Duniani.

Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na wananchi waliofika Uwanja wa ndege wa Zanzibar kumpokea  akitokea  Qatar.  Picha zote: Makame Mshenga - Maelezo Zanzibar.
Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na wananchi waliofika Uwanja wa ndege wa Zanzibar kumpokea akitokea Qatar.
Picha zote: Makame Mshenga – Maelezo Zanzibar.

Qatar yenye wastani wa watu milioni mbili, wengi wao wakiwa ni wageni ni miongoni mwa nchi 10 Duniani vinazoongoza kwa pato kubwa kwa wananchi wake, huku ikiwa ni ya kwanza katika nchi za Mashariki ya Kati.

Chanzo: OMKR

Advertisements

One Reply to “Vijana Zanzibar kunufaika na ajira Qatar”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s