Maji yasumbua Uwanja wa Ndege Z’bar

Znz AirportZanzibar. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar unakabiliwa na mazingira magumu wakati wa mvua kutokana na miundombinu yake kujaa maji na kuwa kero kwa wageni wakiwemo watalii.

Tamko hilo lilitolewa na Waziri wa Habari, Saidi Ali Mbarouk wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano na Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani mjini Zanzibar.

Mwakilishi huyo alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani za kuondosha tatizo la kufurika maji ya mvua katika uwanja huo na kuwapa wakati mgumu wageni na wananchi.

Waziri Mbarouk alisema tatizo hilo limetokana na miundombinu ya kupitishia maji machafu iliyokuwepo ni ya zamani na imeshachakaa na kushindwa kuondosha maji kwa wakati mwafaka kila mvua inaponyesha.

Hata hivyo, alisema hatua iliyochukuliwa na wizara ni kumwita mkandarasi wa Kampuni ya Sogea Satom ili kufanya vipimo na kutayarisha michoro ya kuifanyia marekebisho miundombinu hiyo.

Matokeo ya majanga na mvua za ghafla hayatabiriki, Serikali inaendelea kufanya marekebisho ili kuondoa tatizo hilo hasa kwa kuzingatia uwanja huo ndiyo mlango mkuu wa kuingia wageni na kutoka visiwani humo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s