Polisi: Hatukumpiga risasi Ponda

Muonekano wa jeraha alilolipata Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Muonekano wa jeraha alilolipata Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Morogoro. Shahidi wa pili katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kuwa, hawakuhusika kumpiga risasi mtuhumiwa huyo na kwamba alikamatwa katika Hospitali ya Muhimbili akitibiwa jeraha alilodai lilitokana na risasi.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo shahidi Jafert Kibona, ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Morogoro, alisema Agosti 9, 2013, polisi walipata taarifa kuwa, Sheikh Ponda angekwenda Morogoro kwenye kongamano, hivyo waliwataka waandaaji kumsalimisha polisi kiongozi huyo.

Kibona ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mtwara, alisema polisi walimtaka Sheikh Ponda kujisalimisha kutokana na kutafutwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya kashfa na uchochezi, Dar es Salaam na Zanzibar.

Hata hivyo, Sheikh Ponda alikaidi amri hiyo, badala yake aliendelea kutoa maneno ya kashfa na uchochezi katika kongamano la Morogoro, alidai shahidi huyo mahakamani hapo.

Alidai walishindwa kumkamata Ponda baada ya wafuasi wake kumwingiza kwenye gari dogo na kumtorosha, kabla ya kupata taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kiongozi huyo alijeruhiwa kwa risasi bega la mkono wa kulia.

Kibona alisema walikwenda Hospitali Mkoa wa Morogoro, lakini hawakumkuta Ponda na siku iliyofuata walipata taarifa kuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wakili wa utetezi, Juma Nassoro alimuuliza shahidi huyo kuhusu mtu aliyempiga risasi Ponda, ikiwa polisi ndiyo pekee waliokuwa na silaha siku hiyo.

Aliuliza pia kwa nini polisi walishindwa kumkamata Ponda wakati hakuwa na silaha. Kesi itatajwa tena Februari 2 na 19 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s