Dk Shein apendekezwa kupeperusha bendera ya CCM Urais visiwani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein

Zanzibar. Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar imepitisha azimio la pamoja la kumtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu,imefahamika Visiwani humo.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Fidel Castro na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, huko Pemba.

Alisema kwamba maamuzi hayo yamelazimika kufanyika baada ya kufanyika tathimini na kuona Dk Shein ameonyesha mwelekeo mzuri wa kisiasa na kiuchumi katika kipindi cha uongozi wake kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi baada ya kushika wadhifa huo mwaka 2010.

“Kamati maalum ya Halmashauri Kuu Zanzibar tumepitisha makubaliano na kumuomba aongeze kipindi kingine cha kugombea Urais kwa sababu ametekeleza vizuri ilani ya uchaguzi,  sasa imebakia hiyari yake.”alisema Aboud ambaye  Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho.

Aidha alisema kwamba katika kipindi chake Dk Shein ameonyesha uwezo, busara na hekima kubwa katika kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake ikiwemo kuondoa siasa za chuki na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.

“Wakati ukifika tumekubaliana  katika Kamati Maalum Dk Shein achukuwe fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.”alisema Aboud na kuibua shangwe kwa washiriki wa Kongamano hilo.

Mwaka 2005  Makamo wa Rais Muungano Dk Mohamed Bilal alijitokeza kuchukua fomu na kuchuana na Rais mstaafu Amani Abeid Karume na kuibua hekaheka kubwa ya kisiasa kabla ya kuombwa kuondoa jina lake na wazee kwa madhumuni ya kulinda umoja katika kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s