Adhabu Kwa Waongopao Ndoto, Kusikiliza Siri Za Watu, Wachoraji Picha Zenye Roho

meccaImepokelewa kutoka kwa bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kwamba Mtume (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Anayedai kuwa ameona ndoto ambayo hakuiona, atalazimishwa apige fundo kati ya punje mbili za shayiri, wala hatoweza kufanya hivyo. Na anayesikiliza mazungumzo ya watu na ilhali wenyewe wanachukia, au wanamkimbia [mazungumzo yao asiyasikie], atamiminiwa risasi iliyoyeyuka Siku ya Qiyaamah. Na anayechora picha [ya chenye roho], ataadhibiwa na atalazimishwa aivuvie [aitie] roho wala hatoweza kuivuvia))

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما)عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ تَحَلَّمَ بِحُلْمٍ لَمْ يَرَهُ كُلِّفَ أَنْ يَعْقِدَ بَيْنَ شَعِيرَتَيْنِ وَلَنْ يَفْعَلَ, وَمَنْ اسْتَمَعَ إِلَى حَدِيثِ قَوْمٍ وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ أَوْ يَفِرُّونَ مِنْهُ صُبَّ فِي أُذُنِهِ الأنُكُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ, وَمَنْ صَوَّرَ صُورَةً عُذِّبَ وَكُلِّفَ أَنْ يَنْفُخَ فِيهَا وَلَيْسَ بِنَافِخٍ))   البخاري

Mafunzo Na Hidaaya:

  1. Tisho kali la mwenye kuongopea watu kuhusu ndoto, kwani hivyo ni kumzulia uongo Allaah (سبحانه وتعالى) na watu.

  1. Adhabu kali kwa anayesikiliza siri za watu, nalo ni miongoni mwa madhambi makubwa.

  1. Kusikiliza siri za watu ni miongoni mwa maradhi ya moyo, nayo yanakutokana na kuchunguza mambo ya watu yaliyokatazwa. [Al-Hujuraat 49: 12].

  1. Masikio yanayosikiliza siri za watu, na kila kiungo cha binaadamu kinachotenda maovu, kitakuja kumchongea mtu Siku ya Qiyaamah. [Yaasiyn 36: 65, An-Nuwr 24: 24, Fusw-swilat 41: 20-23].

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا﴿٣٦﴾

Na wala usiyafuate (kusema au kufanya) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo daima vitaulizwa (Siku ya Qiyaamah).

  1. Tisho kali kwa mwenye kuchora picha yenye roho, kwani wanamwiga Muumba kuhusu Uwezo Wake ambao hakuna Awezaye kuumba chochote isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba ni watu watakaopata adhabu kali kabisa [Hadiyth: ((Adhabu kali kabisa ni kwa watu wenye kuchora))].

  1. Kila ‘amali mbovu au nzuri ina malipo yake tofauti.

  1. Mifano ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu kutisha jambo lisilowezekana kutendwa au kutendeka kama kupiga fundo kati ya punje mbili za shayiri. [Al-A’raaf 7: 40, Al-Hajj 22: 73].

Chanzo: Alhidaayah

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s