Kinana apokelewa kwa mabango

Baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Miwani kilichopo Jimbo la Uzini visiwani Zanzibar, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wenye kero zao wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana. Picha: IPP Media
Baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Miwani kilichopo Jimbo la Uzini visiwani Zanzibar, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wenye kero zao wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana.
Picha: IPP Media

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amejikuta akipokelewa kwa mabango na wananchi na kulazimika kuwaagiza viongozi wa chama hicho Mkoa wa Kusini Unguja, na ofisi kuu CCM kusuluhisha mgogoro uliopo kati ya mbunge na mwakilishi wa jimbo la Uzini.

Akizungumza baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa tawi la CCM Miwani, Kinana alisema kutokuwapo kwa maelewano kati ya viongozi hao, kunatishia kukiangusha chama hicho kwa kushindwa kuwapelekea maendeleo wananchi.

Kinana alilazimika kutoa agizo hilo bada ya wananchi wa Miwani na vijiji jirani kumkaribisha kwa kubeba mabango yaliyokuwa na ujumbe kadhaa ukiwamo uliosomeka “Mbunge na Mwakilishi jimbo la Uzini hawaelewani”.

Bango lingine lililalamikia wananchi hao kutokupata huduma muhimu za kijamii kama afya, maji na miundo mbinu ya barabara.

Mbunge wa Uzini ni Dk. Mohamed Seif Khatibu na Mwakilishi ni Mohamed Raza.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM kuwa na umoja na mshikamano, na kutokubali kugaiwa makundi.

Aliwahakikishia wana-CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakiwamo wananchi wa Miwani kuwa malalamiko yao atayafikisha kwa Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete, ili yatafutiwe ufumbuzi, ukiwamo ubovu wa barabara.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema baada ya kumalizika kwa ziara ya Kinana, CCM Zanzibar watafanya tathmini majimbo ambayo yana migogoro na yanaathiri utekelezaji wa Ilani yake na hatua zitachukuwa dhidi ya viongozi wa jimbo ambao hawana maelewano.

“Kama inafikia hatua mpaka wananchi wanabeba mabango kutokana na kutoelewana kwa mbunge na mwakilishi kweli tatizo hilo lipo na hatuwezi kulifumbia macho na naahidi tutalishughulikia,” alisema Nape.

Dk. Khatibu alisema wananchi hao walitumia demokrasia, ingawa alisema hawakupaswa kumeonyesha mabango Katibu Mkuu. Raza hakupatikana kutokana na kuwa safarini nje ya nchi.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s