Katiba Mpya itafungua uchumi wa Zanzibar

Nahodha

Zanzibar. Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha amesema milango ya kiuchumi Zanzibar itafungwa kama Katiba Mpya Inayopendekezwa haitapita katika Kura ya Maoni itakayopigwa Aprili 30, mwaka huu.

Nahodha aliyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Bububu Kwageji, Mkoa wa Mjini Magharibi na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Alisema iwapo wananchi wataamua kuikwamisha kwa kutoipigia kura ya ‘Ndiyo’ Zanzibar itashindwa kupata fursa ya kukopa, kujiunga na Jumuiya za Kikanda na nchi za Visiwa likiwamo Shirikisho la Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) pamoja na kuyaondoa mafuta na gesi katika orodha ya mambo ya Muungano.

“Kama Katiba inayopendekezwa itapita katika kura ya maoni basi milango ya kiuchumi itafunguka Zanzibar kama itakwama, ndoto ya kuondokana na umaskini katu haitatimia,” alisema Nahodha.

Alisema anashangazwa na viongozi wa kisiasa na Serikali wanaofanya kampeni ya kuipinga Katiba Inayopendekezwa wakati Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikilalamika kunyimwa nafasi za kiuchumi. Alisema kitendo cha Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kujitokeza kupinga Katiba hiyo hadharani hakina uzalendo na huruma dhidi ya Zanzibar na kuifananisha hatua hiyo na huruma ya mamba anayekutafuna huku machozi yakimtoka.

“Maalim Seif hana huruma na Wazanzibari, kitendo chake cha kuipinga Katiba Mpya Inayopendekezwa ni sawa na huruma ya mamba anakutafuna huku machozi yakimtoka. Wazanzibari msikubali kufunga milango ya kiuchumi bila kuangali masilahi yetu ya baadaye,” alisema Nahodha.

Wakizungumzia hali ya kisiasa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alishangazwa na urafiki mpya wa CUF na Chadema wakati walibaguliwa wakati wa kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni kutokana na kitendo cha CUF kukubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani humo.

Alisema Chadema waligoma kuunda Baraza la Mawaziri Kivuli na CUF kwa madai chama hicho kimefunga ndoa na CCM na hakuna mwanamke anayekuwa na ndoa mbili kwa wakati mmoja na kuwataka wananchi kuwa makini na vyama vilivyopoteza mwelekeo wa kisiasa.

Akifunga mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwataka wanachama wa CCM Zanzibar kuimarisha umoja na mshikamano wakati huu wa kuelekea katika Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s