Kinana: CCM itahakikisha inashinda uchaguzi Zanzibar

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mlezi wa CCM  Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi kwenye afisi ya CCM Wilaya ya Dimani, Kiembe Samaki Zanzibar
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi kwenye afisi ya CCM Wilaya ya Dimani, Kiembe Samaki Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Abdulrahman Kinana, amesema atatoa kila msaada kuhakikisha CCM inashinda Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Alisema hayo wakati akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika visiwani hapa ikiwa ni miongoni mwa ziara zake.

Alisema ikiwa yeye ndiyo katibu mkuu wa chama hicho atahakikisha anatoa kila msaada CCM  kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo katika ngazi za uraisi, uwakilishi, ubunge na udiwani.

Aliwataka wanachama hao kuanza kutembea kifua mbele na wasiwe wanyonge kwani ushindi ni lazima kwa CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Alisema tangu ameanza ziara zake za kichama Zanzibar kukaguwa utekelezaji wa ilani ya CCM na kukiimarisha chama visiwani hapa, ameridhishwa na utendaji kazi wa viongozi katika chama hicho kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa ufanisi mkubwa.

Alisema ziara yake iliyoanza wilaya ya mjini , amethibitisha kuwa CCM mjini ipo imara , wanachama wake wanaumoja, ari, ushirikiano na wako tayari kulitumikia taifa.

Akizungumzia kuhusu katiba iliyopendekezwa alisema hana shaka na katiba hiyo kwani wananchi wataifahamu, wataielewa ,wataikubali na wataipigia kura ya ndiyo.

Alisema  ni nzuri inawafaa Watanzania wote wala haina matatizo imeiingiza masuala muhimu .

“ Wana – CCM endeleeni na mshikamano msikubali kugawanywa na niwahakikishieni ccm itashinda katika uchaguzi mkuu na katiba iliyopendekezwa itapita kwa kura nyingi za ndiyo” alisema Kinana.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha,  alisema viongozi wa vyama vya upinzani wanapita kusema uongo na kuwaambia wananchi waikate katiba hiyo na kusema kuwa kitendo hicho ni cha upuuzi.

“Niwaambie wanachama wa CCM na wananchi watu hao siyo wakweli wana ndimili kwani wakiwa hadharani wanasema wanaunga mkono mfumo wa serikali tatu lakini wakiwa katika vikao vyao vya ndani wanaunga mkono serikali ya mkataba,” alisema Nahodha.

Alieleza kuwa  kwa muda mrefu Wazanzibari walikuwa wakilalamika hawapati kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) na kwamba  katiba iliyopendekezwa itawapa  Wazanzibari  fursa ya kujiunga.

Aliwataka wanachama wa CUF kama wanania ya dhati ya kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mkuu wawape Chadema majimbo Pemba kwani wakifanya hivyo ndiyo watakuwa na umoja wa dhati katika umoja wao.

“Sijapata kuona paka na panya wakashirikiana na endapo watashirikiana itakuwa majaabu ya ngamia kupita katika tundu ya sindano” alisema Nahodha.

Mwakilishi wa Kwamtipura, Hamza Hassan Juma, alisema endapo katiba iliyopendekezwa itapita Zanzibar itaweza kuzalisha umeme yenyewe kwani sasa inanua umeme kutoka Tanzania Bara.

Chanzo: Nipashe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s