Sheikh akoromea siasa za kuchafuana

Sheikh aonya fursa ya uhuru wa kuzungumza isitumike vibaya, kwa kuwa athari zake ni kubwa.
Sheikh aonya fursa ya uhuru wa kuzungumza isitumike vibaya, kwa kuwa athari zake ni kubwa.

Dodoma. Wanasiasa nchini wametakiwa kuachana na siasa za kufanya kampeni za kuchafuana kwa ajili ya kuwashawishi wananchi wawachague, kwa kuwa muda ukifika wale wanaohitajika ndiyo watakaochaguliwa.

Onyo hilo lilitolewa mjini hapa jana na Sheikh Ahmad Zuberi wa Msikiti wa Sunni Muslim Jamaat Jumaa, alipozungumzia nafasi ya wananchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na rais.

Sheikh Zuberi alisema tabia ya wanasiasa kujihusisha katika kampeni za kuwataka wananchi wawachague inaweza kusababisha kutowapata viongozi watakaowajali wananchi, badala yake wale wakakaowatumikia waliowaweka madarakani.

“Ni vyema viongozi wenye tabia hiyo chafu wakaiacha na kutoa fursa kwa wananchi wenyewe kuamua ni kiongozi gani anayeweza kuwasaidia katika kusikiliza na kutatua kero zao zinazowasibu kila siku,” alisema Sheikh Zuberi.

Alisema wakijiandikisha na kupiga kura wanaweza kufanya uamuzi mzuri utakaowawezesha kuwapata viongozi wenye kuwajibika, utii na uchungu kwa wananchi na Taifa.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Ahmed Ame aliwataka Watanzania kujiepusha na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa lengo ya kuchafuana.

Alisema hivi sasa mitandao hiyo badala ya kutumika kwa malengo maalumu, imegeuka kuwa adui ikiwamo kutumiana picha zisizo na maadili na zinazopotosha umma hususan vijana.

“Vijana wetu sasa hivi, muda mwingi wapo kwenye kutafuta vitu kwenye simu zao na vitu wanavyoangalia ni vya aibu kwa Taifa letu na hata kwa wazazi,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s