‘Hatufukuzi mgombea urais CCM’

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM , mjini Unguja , Zanzibar jana.  Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein .
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM , mjini Unguja , Zanzibar jana. Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

Zanzibar. Wakati Kamati Kuu ya chama tawala, CCM ikimaliza vikao vyake mjini hapa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana amesema mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu baadhi ya wanachama wanaotajwa kuwania urais hayana ukweli, wala hakuna atakayefukuzwa uanachama.

Kinana aliyasema hayo jana mjini hapa kuhusu mambo yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi za urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, Oktoba.

Kamati Kuu ya CCM hadi jana jioni ilikuwa ikiendelea na kikao chake kwenye ofisi kuu ya chama, Kisiwandui, Zanzibar.

Kauli ya Kinana imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono kuwa baadhi ya makada waliojitokeza kutangaza ama kuonyesha nia kuutaka urais watachukuliwa hatua, zikiwamo kutimuliwa.

“Mambo yanayozungumzwa ni mengi kuwa baadhi ya wagombea majina yao yatakatwa. Hayo ni majungu ya kisiasa, yamelenga kuwachokoza viongozi na chama ili wapate cha kusema.

“Chama kina utaratibu na uamuzi unaofanyika kwa vikao maalumu, hizi ni propaganda, ni uchokozi kwa chama chetu,” alisema Kinana.

Wakati Kinana akijaribu kuwaondoa hofu vigogo wanaowania nafasi hiyo, tayari wagombea hao wamepiga kambi mjini hapa, baadhi yao wakiendesha kampeni za chini chini, tangu kumalizika kwa sherehe za Mapinduzi visiwani hapa juzi.

Wagombea hao wamekuwa wakipishana kuingia visiwani na kukutana na baadhi ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM na mkutano mkuu kila upande ukijiimarisha kisiasa kabla ya mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia chama hicho Mei mwaka huu.

Vikumbo mitaani

Katika hoteli kadhaa mjini hapa baadhi ya makada wamekuwa wakipigana vikumbo ikiwa ni hatua ya kuweka mikakati ya kutengeneza mazingira, hasa ya kukubalika katika chama hicho.

Hata hivyo, tofauti na vikao vingine vya chama hicho tawala, idadi ya wapambe wa makundi yanayotajwa kuwania urais waliofika mjini hapa imekuwa ni ndogo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s