Miaka 51 ya Mapinduzi, hakuna wodi maalum ya watoto

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole mtoto mgonjwa Nasrya Kombo aliyelazwa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuungua kiwa moto. Pembeni ya Balozi Seif ni Muuguzi wa Zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya Watoto Bibi Mary Jadi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole mtoto mgonjwa Nasrya Kombo aliyelazwa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuungua  moto. Pembeni ya Balozi Seif ni Muuguzi wa zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya watoto Bibi Mary Jadi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar ina nia ya kutaka kujenga wodi  maalum kwa ajili ya  kulazwa watoto wadogo wanaopatwa na majanga  mbali mbali ya kuungua kwa moto.

Balozi Seif alisema hayo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua watoto walioungua moto ambao wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaelewa vizuri matatizo yanayowakumba watoto wanaopatwa na majanga hayo ya moto ambao hulazimika kulazwa  zaidi ya mtoto mmoja kwenye kitanda kimoja.

Muuguzi wa zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya Watoto Bibi Mary Jadi akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif msongamano wa watoto wanaoungua moto ambao hulazimika kulazwa wagonjwa watatu kwa kitanda kimoja.
Muuguzi wa zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya Watoto Bibi Mary Jadi akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif msongamano wa watoto wanaoungua moto ambao hulazimika kulazwa wagonjwa watatu kwa kitanda kimoja.

Balozi Seif alisema hali hiyo mbali ya kwamba haipendezi  kuonekana lakini pia inaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mbali mbali kwa watoto wanaolazwa pamoja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wazazi na walezi kuwa waangalifu na matukio ya majanga ya  moto ambayo huonekana  kushamiri zaidi katika baadhi ya vipindi na kusababisha vifo na hata vilema kwa watoto wao.

Mapema Muuguzi wa zamu wa wodi ya watoto katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Bibi Mary Jadi alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ajali za moto zinazowakumba watoto katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku.

Balozi Seif akimpa pole Bibi Wanu Rajab aliyelazwa Hospital Kuu ya Mnazi mmoja yeye na mtoto wake baada ya kibanda wanachoishi katika shughuli za kilimo kuwaka moto katika Kijiji cha Kilombero.
Balozi Seif akimpa pole Bibi Wanu Rajab aliyelazwa Hospital Kuu ya Mnazi mmoja yeye na mtoto wake baada ya kibanda wanachoishi katika shughuli za kilimo kuwaka moto katika Kijiji cha Kilombero.

 Bibi Mary alisema ipo haja ya kufanywa kwa utafiti wa kina kuelewa sababu zinazopelekea kuongezeka kwa majanga hayo  na juhudi zifanywe kwa makusudi ili kupunguza au kuondosha kabisa tatizo hilo ambalo huonekana kushamiri zaidi katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Chanzo: OMPR

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s