Maandamano ya kutowastahamili, kutowaridhia wageni Ujerumani

Wananchi wa Ujeumani waliokamata mabango kupinga wageni na uislamu wenye siasa kali
Wananchi wa Ujeumani waliokamata mabango kupinga wageni na uislamu wenye siasa kali

Na Othman Miraji

Kuna hatari ya kuenea chuki dhidi ya raia wa kigeni Ujerumani. Hisia dhidi ya Uislamu zimezidi siku hizi katika nchi hiyo. Kumekuwa kukiripotiwa matukio ya kushambuliwa misikiti na makazi ya wahamiaji. Visa hivyo vinatokana na kuundwa kwa vuguvugu lenye jina la PEGIDA, yaani Wazalendo wa Ulaya wanaopinga kuenea Uislamu katika nchi za Magharibi.

Kundi hilo lilianzia mjini Dresden likiwa lina watu 300, lakini sasa linajivunia wanachama wanaokaribia 20,000 nchini Ujerumani. Kundi hilo hufanya maandamano kila Jumatatu katika miji tofauti huku likiwa limebeba mabango yenye maandishi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni na pia kuupinga Uislamu.

Visa vya kuwachukia raia wa kigeni vimekuwa vikizidi, hali inayoashiria kwamba wananchi wa Ulaya wanazidi kuelemea katika siasa za mrengo wa kulia. Mambo yalikuwa kama hivi; raia wa Norway, Anders Behring Breivik, alipofanya mauaji mjini Oslo mwaka 2011, kwanza alilipua bomu mbele ya majengo ya Serikali na baadaye akaishambulia kambi ya tawi la vijana ya chama tawala cha Labour. Aliua watu 77, akidai kwamba amefanya hivyo kutokana na msimamo wake dhidi ya Uislamu, pia kupinga kuweko mchanganyiko wa tamaduni mbalimbali nchini Norway.

Chuki

Chuki dhidi ya raia wa kigeni huchochewa na wanasiasa. Kwa mfano, chama cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa ambacho sasa kinaongozwa na Marine Le Pen kilikuwa ni chama kidogo katika miaka ya themanini na kilikuwa kati ya vyama vya mwanzo kuushutumu Uislamu na kutaka raia wa kigeni warejeshwe makwao.

Hivi sasa Bibi Le Pen ni mtetezi ambaye huenda akaongoza katika uchaguzi wa urais mwaka 2017.

Siasa dhidi ya Uislamu na kuwachukia wageni ni bidhaa inayouzwa kwa urahisi hivi sasa na wanasiasa wa mrengo wa kulia sana katika nchi kadhaa za Ulaya.

Kweli, usasa na utandawazi umeharakisha kuja kwa mabadiliko ya kijamii tunayoyaona na ambayo pia yanasababishwa na idadi kubwa ya watu wanaohama kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Hali hiyo inasababisha kuwako na hofu miongoni mwa watu wa nchi yeyote kwamba huenda wakapoteza utambulisho wao na kile walicho nacho.

Ni kawaida kwamba inajengeka chuki pale panapokuwako kundi la watu walio nacho na kundi jingine la watu wasiokuwa nacho.

Iko hofu kwamba maelfu ya wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati na Afrika, wanaovuka Bahari ya Mediterania, wanaingia Ulaya kuwapokonya au kuwapunguzia wazawa wa Ulaya neema walio nayo.

Hivyo, inafaa wazuiwe, pia bahari hiyo ya Mediteranea igeuzwe kuwa ukuta usiopitika baina ya Afrika na Ulaya.

Nchi nyingi za Ulaya zina neema, hasa Ujerumani, ukilinganisha na nchi nyingi nyingine nje ya bara hilo. Wazawa wa nchi za Ulaya hujisifu kwamba neema yao inatokana na mfumo wao wa utawala wa demokrasia na usasa.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s