Balozi Seif: Tutayalinda Mapinduzi kwa nguvu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akivishwa skafu na vijana wa chipukizi wa CCM kabla ya kuzindua matembezi ya UVCCM kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Unguja Ukuu.Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Nd. Sixtus Mapunda na kushoto yake ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Shaka Hamdu Shaka
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akivishwa skafu na vijana wa chipukizi wa CCM kabla ya kuzindua matembezi ya UVCCM kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Unguja Ukuu.Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Nd. Sixtus Mapunda na kushoto yake ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Shaka Hamdu Shaka

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seid Ali Idd, amesema serikali itakuwa tayari kupambana na mtu au kikundi chochote kitakachothubutu kuharibu Mapinduzi.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye ufunguzi wa matembezi ya Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema serikali ya Mapinduzi ni ya wananchi wenyewe ambao hawako tayari kuona uhuru na ukombozi wao ukipuuzwa na watu wachache kwa ajili ya maslahi yao.

Alisema kuwa serikali ya Zanzibar bado ipo imara wakati wowote na wapo makini dhidi ya chokochoko zozote.
“Tunashangaa baadhi ya watu sasa waliokataa kuyatambua Mapinduzi, sasa  nao wanaimba nyimbo za kusifu kwa unafiki,” alisema Balozi Seif bila kuwataja.

Balozi Self alisema unafiki wa watu hao hujidhihirisha kutokana na vitendo vyao kwa kuwa wanayoyasema ni mambo tofauti na yale yaliyoko kwenye mioyo yao na kuwataka wananchi wa Zanzibar kuwa macho na watu hao.

Aidha Muungano, alisema kitendo chochote cha kudhoofisha Muungano kamwe kisipewe nafasi kwani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si wa makaratasi bali ni damu.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s