Safari ya demokrasia Zanzibar haijaanza

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein
                                 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein

Na Salim Said Salim

Mara nyingi nimeeleza kuwa safari ya kuelekea kwenye utawala wa kidemodrasi, wa haki na sheria Zanzibar ni ndefu na iliyojaa milima na mabonde, matope na kila aina ya vizingiti na vikwazo.


Lakini kwa namna mambo yanavyoendelea Visiwani hivi sasa inaonekana ni sawa na kusema safari haijaanza na nia ya kuianza  haipo.
Badala yake tunaona vitendo na kusikia kauli zilizozoeleka katika nchi ambazo udikteta umetawala na waliopo madarakani hataki kuona wananchi wanatendewa haki.


Taarifa za hivi karibuni zimeonyesha kwamba watu wapatao 250,000 wa Unguja na Pemba hawataweza kushiriki katika kura ya kuamua kuikubali au kuikataa hio katiba iliyopitishwa kwa njia ziliojaa mzozo, ikiwa pamoja na kuambiwa maiti walipiga kura katika Bunge la Katiba, wala kushiriki katika uchaguzi mkuu.


Sina mashaka na taarifa hii kwa sababu hata katika familia yangu wapo watu wengi ambao wananyimwa haki ya kupiga kura wakati waliokuja Zanzibar wakati wa mbio za mwenge au sherehe za Paska na kubaki Visiwani wanayo haki hio.


Watu wengi waliozaliwa nakuishi Zanzibar hawataweza kuandikishwa kuwa kupiga kura kwa vile hawana vyeti vya kuzaliwa.


Vyeti hivi ambavyo huwa havipatikani kwa urahisi ardhini wala mbinguni ndio vinayomuwezesha mtu kupata haki ya kuandikishwa kuwa Mzanzibari. Baadaye huyu mwenye cheti hicho kamae akibahatika kwa ridhaa ya sheha ndio hupewa haki ya kuandkishwa kupiga kura.


Vile vile si ajabu hata akiandikishwa jina lake likawa haimo katika dafatari la kupiga kura au kufukuzwa kwenye mstari wakati akisubiri kupiga kura.


Matokeo yake ni kwamba wapo maelfu ya watu ambao wao na wazee wao wamezaliwa na kuishi Zanzibar wamekuwa wanaishi Visiwani kama vile ni wakimbizi au watalii.


Wakati zama za ukoloni ilikuwa rahisi kukipata cheti cha kuzaliwa siku hizi za Mapinduzi Daima mtu anaweza kuhangaika kwa miaka kukipata, tena kwa shilingi 35,000,kiwango cha fedha ambacho masikini hana uwezo wa kukipata kwa urahisi.


Naelewa fika kuwa maelezo haya hayatawafurahisha wale wanaoweka vikwazo hivi, zaidi kwa sababu ya kisiasa.
Lakini ukweli lazima usemwe na chombo cha habari kinachoufumbia macho masuala kama haya huwa kimeshindwa kutekeleza wajibu wake na zaidi kama sauti ya wanyonge.


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mekuwa ikiahidi kutandika mazingira mazuri ya mfumo wa demokrasia, lakini kinachoonekana ni tafauti.
Watu wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi kaa za kupiga kura na wengine kutukanwa na kukashifiwa hadharani na hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa wanaofanya uhuni huu.


Mabao ya matangazo ya CCM, hasa lamaskani ya Kisonge, handika inachokitaka na hakuna anayewaambia lolote kama vile mabwana na mabibi wakubwa wa maskani hii wapo juu ya sheria za nchi.


Wapo wtu wanaothubuu kutoa kauli za uchochezi za kusema wanaotaka kuleta mabadiliko Visiwani wasitegemee  hayo kufanyika kupitia uchaguzi.


Badala yake watu hao hutakiwa wal Busiady na serikali yake ya mseto ya ZNP na ZPPP.Wanaotoa kauli hizi hawaulizwi lolote lile kama vile matamshi hayo sio mabaya.


Lakini kama patatokea wapinzani kutoa kauli kama hizo za uchochezi tungeliona polisi wanavyohangaika huku na huko na kusaka wliosema hayo na kesi kufunguliwa haraka haraka na watuhumiwa kusukumwa gerezani baada ya kunyimwa dhamana.


Si ajabu baadhi ya watu hao wakafunguliwa mashitaka ya ugaidi na kuhusishwa na vikundi vya kimataifa vya ugaidi.
Hii ndio hali halisi ya Zanzibar na wapo watakonuna ukweli huu ukisemwa, lakini hama hawataki haya yazungumzwe wasingeliyafanya.


Safari ya mwaka 2015 ambayo itakuwa na kura juu ya hio katiba mpya ( sio ile iliyopendekezwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba kutokana na maoni ya wananchi) na uchaguzi mkuu.


Tayari hali ya kisiasa Visiwani imeanza kuonyesha ishara ya kuwa tete na kila unaposikia ahadi za serikali za kuhakikisha amani na utulivu ndio utaona wananchi wanabanwa zaidi na kunyimwa haki ya kupiga kura na wengine kuruhusiwa kubagua na kutukana watu.


Zanzibar tokea kuanza tena mfumo wa vyama vingi vya siasa zaidi ya miaka 20 iliopita imepitia misukosuko mingi na watu kupoteza maisha yao, wakiwemo wale walikuwa wanapacheka bendera ya kufungua tawi la chama chao.
Wengi tulidhani wana siasa wetu, waliop madarakani na wa kambi ya upnzani, watajifunza kutokana na makosa yaliyotokana na siasa za chuki na uhasama.


Kwa bahati mbaya inaonekana kwamba yaliyotokea siku za nyuma mpaka pakaundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) bado hayajatoa somo.
Sijui kinangojewa nini kitokee ndio watu wajifunze kwamba siasa za uhasama na kunyima watu hai zao za kiraia na kibinaadamu ni vibaya na husababisha hatari na athari.


Katika salamu zao za Mwaka Mpya Marais Jakaya Kikwete (Muungano) na Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) wwaliwataka wananchi kudumisha amani na umoja.


Huu ni wito mzuri hasa wakat huu tunapoelekea kwenye kura ya maoni juu ya katiba na uchaguzi mkuu.


Lakini…lakini…lakini.. ikumbukwe kuwa amanai na utulivu hupatikana pale penye utawala wa haki na sheria na amani hutoweka pale ambapo baadhi ya wana jamii huona hawatendewi haki na wanadhulumiwa.
Ni vizuri kwa kasoro hizi zinazoonekana za utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, kuwapatia wananchi haki ya kujiandikishwa kama Wazanzibari na hatimaye kuweza kupiga kura zirekebishwe haraka.


Nchi nyngi ziliowabana watu wake kama inavyoonekana Zanzibar hivi sasa zimekuwa na matokeo mabaya. Ni vizuri pakafanywa juhudi sio za kucukua tahadhari ya hayo kutokea Visiwani, bali hata kukaribia.


Sheria za nchi laizma ziaachiwe kuchukua mkondo wake. Polisi wawasake na kuwawajibishwa wanaotukana na kukashifu watu  kama sheria zinavyotaka.


Mahakama nazo zifanye kazi yake na kuonekana kama eneo la kukimbilia kutafuta haki na sio kutumika, kama baadhi ya watu wanavyoona na kuamini, kuwa ni vitengo vinavyotumika  kunyima watu haki zao za kikatiba na kibinaadamu.


Hisi sio tena zama za kutawala kwa kutumia mabavu na misuli au kuzigeuza sheria juu chini ili kukidhi utashi wa kisiasa. Hata ukifukuza watu makazini au shule kwa sababu tu walitaka kupiga kura kama ilivyofanywa na serikali miaka ya nyuma haisaidii.


Upepo wa mageuzi ukivuma huwa hauzuiliki kama ule wa Tsunami.Kujaribu kuzuwia maji kujaa nakukupwa nikujidanganya.
Tumeona namna walivyoadhiriki viongozi wa nchi mbali mbali waliofikiri mabavu na mauaji yangeliwasaidia kuwakandamiza wananchi na ktawala kwa namna watakavyo.


Upo usemi miongoni mwa wana jamii wa Bohemia  (watu wa Jamhuri ya Czeh, hasa wale wanaoishi kando ya Mto Danube) unaoeleza kwamba pale jani kavu linapoanguka hilo huwa onyo kwa majani mabichi yaliobaki kwenye mti.


Mpaka pale patapoonekana nia njema ya kuwa na demokrasia ya kweli na viogozi wote wa  kisiasa wa Zanzibar kuamua kuweka maslahi ya nchi mbele na sio yao binafsi au kuwekeana kisasi maendeleo ya kweli Visiwani na hasa ya utawala wa haki na sheria yatabaki kuwa ndoto.


Ni vizuri kwa kila mtu kuelewa anapojikwaa na kujaaliwa kuinuka na kuanza teana kwenda basi achukuwe tahadhari katika safari yake asije kuanguka.


Mwisho ya yote kila mtu afahamu vyama vya siasa ni vya muda, lakini Zanzibar itabaki na ni mali ya watu wote wa Unguja na Pembana sio chama chochote kile cha siasa.


Wale ambao hawalikubali hili ndio wahame na watafute pa kwenda na sio kuwa na jeuri ya kuwaambia wenzao wahame na kwenda eneo ambalo hawana nasaba nalo.Tujirekebishe kwa maslahi ya Zanzibar ya leo na siku zijazo.

Chanzo: Tanzania Daima

Advertisements

One Reply to “Safari ya demokrasia Zanzibar haijaanza”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s