Maalim Seif: Tunatarajia ushindi mkubwa mwaka huu

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia wanachama wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mapembeani, mjini Zanzibar
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia wanachama wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mapembeani, mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwa namna chama hicho kilivyojipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba kuna matarajio makubwa kitapata ushindi sichini ya asilimia 70 ya kura za Urais, viti vya Ubunge, Uwakilishi pamoja na Udiwani.

Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mapembeani, jimbo la Mji Mkongwe, baada ya kukabidhi mashine tisa za boti za kuvulia samaki na fedha taslim shilingi milioni 27 zilizotolewa na Mbunge wa Mji Mkongwe, Mohammed Ibrahim Sanya kwa ajili ya matawi ya CUF jimboni humo.

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi fedha taslim shilingi milioni 27 kwa viongozi wa matawi ya CUF, katikia jimbo la Mji Mkongwe zilizotolewa na Mbunge wa jimbo hilo Mohammed Sanya
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi fedha taslim shilingi milioni 27 kwa viongozi wa matawi ya CUF, katikia jimbo la Mji Mkongwe zilizotolewa na Mbunge wa jimbo hilo Mohammed Sanya

Maalim Seif amesema miongoni mwa mikakati kabambe itakayokipa ushindi mkuba CUF ni mpango wake wa kuzigawa Wilaya mbili za Mjini na Magharibi katika zoni mbili mbili, hatua ambayo itakiwezesha chama hicho kuratibu shughuli zake ikiwemo uchaguzi kwa urahisi zaidi.

Maalim Seif alisema Wilaya ya Magharibi ambayo ina jumla ya majimbo tisa ya uchaguzi imegawiwa katika zoni za Mfenesini na Dimani, wakati Wilaya ya Mjini yenye majimbo 10, imegawiwa katika zoni za Mjini na Amani.

“Chama cha CUF tumeandaa mikakati kabambe na tuna matarajio ya kupata ushindi mkubwa wa asilimia 70 kura za Urais, asilimia 70 viti vya Ubunge na Uwakilishi na asilimia 70 viti vya Udiwani”, alisema Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi mashine za boti za kuvulia samaki zilizotolewa na Mbunge wa Mji Mkongwe, Mohammed Sanya kwa wananchi wa jimbo hilo
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi mashine za boti za kuvulia samaki zilizotolewa na Mbunge wa Mji Mkongwe, Mohammed Sanya kwa wananchi wa jimbo hilo

Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema Chama cha Mapinduzi hivi sasa tayari kinakabiliwa na msukosuko mkubwa wa kukimbiwa na wanachama wake wanaojiunga na CUF na tayari chama hicho tawala kimeanza kuona dalili za kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Maalim Seif alisema baada ya kuona hali hiyo hivi sasa CCM kimeanza kuchanganyikiwa na kufanya mbinu chafu, ikiwemo kuwaweka vijana kwenye makambi ili waje waweze kuwasaidia kushika madaraka katika uchaguzi mkuu huo.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema mbinu hizo hazitafua dafu, kwa sababu wananchi walio wengi Zanzibar wakiongozwa na vijana tayari wamekikataa chama hicho cha CCM na hakutakuwa na mbinu wala hila zitakazowawezesha kushinda.

“Katika nchi yoyote ile vijana wakishaamua basi jambo wanalolitaka ndilo linalokuwa, CCM mmejitakia wenyewe, wimbi hili ni kubwa na wala hamuwezi kulizuia”, alisema Maalim Seif.

Wiki iliyopita, CUF kilizoa wanachama wapya 108 wakiwemo waliohama CCM ambao walipokelewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Pje, Wilaya ya Kusini Unguja. Miongoni mwa anachama wapya waliopewa kadi ya CUF katika mkutano huo ni aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mansour Yussuf Himid, ambaye alitimuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi.

Viongozi na wanachama wa CUF wa Mji Mkongwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, baada ya kukabidhi fedha taslim na mashine tisa za boti za kuvulia samaki kwa wananchi wa juimbo hilo
Viongozi na wanachama wa CUF wa Mji Mkongwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, baada ya kukabidhi fedha taslim na mashine tisa za boti za kuvulia samaki kwa wananchi wa juimbo hilo. Picha zote: OMKR

Aidha, Maalim Seif amelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria na wajiepushe kutumiwa vibaya na CCM, hasa wakati wa uchaguzi mkuu.

Alieleza kuwa mara nyingi vijana wanaoandaliwa kufanya vurugu na kukisaidia CCM hupata nguvu kutokana na kulindwa na kusindikizwa kwa magari ya Polisi kufanya maovu hayo, jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za jeshi hilo.

Katika hafla hiyo, Mbunge wa Mji Mkongwe, Mhe. Mohammed Ibrahim Sanya amewataka vijana wa Zanzibar kujiweka tayari kulinda ushindi mkuba wa chama hicho ambao hauna shaka yoyote katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba na ili kumuwezesha Maalim Seif kukamata Ikulu ya Zanzibar akiwa Rais.

Chanzo: OMKR

Advertisements

One Reply to “Maalim Seif: Tunatarajia ushindi mkubwa mwaka huu”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s