Balozi Seif: Mnaoishi kwenye nyumba mbovu muhame

Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia nyumba iliyoporomoka dari na kujeruhi wakazi wake watatu hapo mtaa wa Ukutani mjini Zanzibar. Kushoto mmiliki wa nyumba hiyo bwana Mzee Abdulla Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia nyumba iliyoporomoka dari na kujeruhi wakazi wake watatu hapo mtaa wa Ukutani mjini Zanzibar. Kushoto mmiliki wa nyumba hiyo bwana Mzee Abdulla Juma.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewaagiza wananchi wanaoishi kwenye nyumba  mbovu na zile zilizochakaa ndani ya Mji Mkongwe  wa Zanzibar wafanye utaratibu wa kuhama kwenye nyumba hizo mapema iwezekanavyo ili kunusuru maisha yao.

Alisema Serikali kamwe haitakuywa tayari kuachia wananchi wake  wanaoendelea kuishi katika mazingira ya hatari wakati njia za kuepuka hatari hizo zipo na wala hazina gharama yoyote.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua nyumba ya bwana Mzee Abdulla Juma ambayo iliporomoka dari sehemu ya sebule na kujeruhi wakaazi watatu wa nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Ukutani mjini Zanzibar.

Watu waliojeruhiwa ni wadogo wa mmiliki wa nyumba hiyo Bw. Haroun Abdulla Juma na Fahim Abdulla Juma waliolazwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu pamoja na Peter Monga aliyetibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

 Balozi Seif aliutaka uongozi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kuendelea kuzifanyia uhakiki nyumba zote zilizomo ndani ya Mji Mkongwe na hatua zichukuliwe mara moja na taasisi zinazohusika katika kuwahamisha wakaazi wanaoishi kwenye nyumba zisizostahili kuishi watu.

UkutaniMapema mmiliki wa nyumba hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mkasa huo umetokea majira ya saa 11.00 za asubuhi wakati dari ya nyumba hiyo sehemu ya sebule ilipoporomoka.

Bwana Mzee alisema wakaazi wa nyumba hiyo kwa kushirikiana na majirani walilazimika kuuvunja mlango mkuu wa nyumba hiyo ili kumnusuru mtoto wa mdogo wake aliyelazwa hospitali kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuvunjika mguu.     

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd.   Mussa Awesu Bakari alisema watendaji wa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa taasisi za majengo na ujenzi tayari wameshafanya uhakiki wa nyumba 75 zilizomo ndani ya Mji Mkongwe .        

Nd. Mussa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba  zoezi hilo linaendelea kwa lengo la kubaini nyumba zisizofaa kutumiwa kwa makazi ya kawaida ya binadamu.

Chanzo: OMPR

One Reply to “Balozi Seif: Mnaoishi kwenye nyumba mbovu muhame”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s