Polisi yashikilia wawili kwa ujambazi Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano Nyumbani kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kuvamiwa na majambazi jana usiku yeye na wenzake  maeneo Vuga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano Nyumbani kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kuvamiwa na majambazi jana usiku yeye na wenzake maeneo kati ya Kikwajuni na Suza, Vuga.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi  Msaidizi Kamishna wa Polisi (ACP) Mkadam Khamis Mkadam alisema Jeshi la Polisi Mkoa huo linawashikilia  watu wawili  miongoni mwa majambazi wanaotuhumiwa kuhusika na uvamizi wa Madaktari Bingwa wa Cuba  katika maeneo kati ya Kikwajuni Wireles na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) mapema jana usiku.

Alisema polisi ilianza uchunguzi mara moja baada ya kupata taarifa ya kuvamiwa kwa Madaktari hao walionyang’anywa mikoba, vitu mbalimbali pamoja na fedha zao  ambapo mmoja kati yao Profesa Ulpiano alijeruhiwa kwa panga kichwani.

Balozi Seif akibadilishana mawazo na Madarkati wa Cuba hapo nyumbani kwao Vuga alipokwenda kuwafariji na kuwapa pole baada ya kuvamiwa na Majambazi.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na madarkati wa Cuba hapo nyumbani kwao Vuga alipokwenda kuwafariji na kuwapa pole baada ya kuvamiwa na Majambazi.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mkadam Khamis Mkadam alieleza hayo wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alipofika nyumbani kwa Madaktari hao Vuga Mjini Zanzibar kuwafariji baada ya kupatwa  na mkasa huo.

Kamanda Mkadam alisema Mkoa wa Mjini umekuwa na matukio ya kuibuka kwa vitendo vinavyoashiria kuichezea amani baadhi ya wakati jambo ambalo jamii inahusika kwa kiasi kikubwa katika kushirikiana na Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo hivyo.

Alisema ulinzi ni jukumu la watu wote, hivyo miundo mbinu iliyopo hivi sasa duniani ya mitandao ya mawasiliani katika uwekaji wa kamera za CCTV inahitajika kutumika kwa lengo la kuwabaini watu wanaojihusisha na matendo maovu.

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi alizishauri Taasisi za umma, binafsi na hata watu wa kawaida wakakijengea utamaduni wa kutumia mfumo huo mpya ili kuwa na maisha  ya salama.

Akiwapa pole madaktari hao bingwa wa Cuba wanaotoa huduma katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na kusomesha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hilo ni tukio la ajabu na la kusikitisha katika visiwa vya Zanzibar.

Balozi Seif alisema vitendo hivyo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wahuni vimekuwa vikileta sura mbaya kutokana na  sifa ya Zanzibar yenye utamaduni wa kistaarabu wa kupenda wageni tokea karne nyingi zilizopita.

Madaktari wa Cuba waliovamiwa na majambazi kutoka kushoto ni Mke wa Madaktari hao Dk. Ulpiano, Dk. Katia na Dk. Barbara
Madaktari wa Cuba waliovamiwa na majambazi kutoka kushoto ni Mke wa Madaktari hao Dk. Ulpiano, Dk. Katia na Dk. Barbara

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Madaktari Bingwa hao wa Cuba kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake vya ulinzi inaendelea na uchunguzi wa kina na wahusika wa vitendo hivyo watakapo patikana mkondo wa sheria utafanya kazi zake dhidi ya wahalifu hao.

Balozi Seif aliwataka Madaktari hao kuendelea na majukumu yao kama kawaida na Serikali itakuwa makini katika kuwahakikishia usalama wao pamoja na wageni wengine wakati wao wote wawapo hapa nchini.

Wakitoa shukrani zao kwa faraja hiyo pamoja na juhudi zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi katika kuwasaka wahalifu waliohusika na tukio hilo madaktari hao wa Cuba waliahidi kuendelea kutoa huduma kama kawaida licha ya mkasa uliowakumba.

Madaktari hao walielezea matumaini yao kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya ulinzi  vitafanya juhudi za ziada katika kuona kwamba matukio kama hayo yanadhibitiwa kabisa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na mke wa kiongozi wa madaktari wa Cuba Dk. Ulpiano mara baada ya kuwapa pole kutokana na mtihani uliowapata wa kuvamiwa na majambazi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na mke wa kiongozi wa madaktari wa Cuba Dk. Ulpiano mara baada ya kuwapa pole kutokana na mtihani uliowapata wa kuvamiwa na majambazi

Madaktari  hao wanne wa Cuba ni Dk. Barbara, Dk. Daisy Battle, Dk.Katia wakiwa na Kiongozi wao Profesa Ulpiano walivamiwa ghafla na vijana walioshuka  na mapanga kwenye Gari aina ya Noah wakati wakitokea  Kikwajuni kuelekea nyumbani kwao Vuga.

Chanzo: OMPR

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s